Loading...
title : Msimshambulie Magufuli kukataza Wenye Ujauzito Warudi shuleni-Askofu
link : Msimshambulie Magufuli kukataza Wenye Ujauzito Warudi shuleni-Askofu
Msimshambulie Magufuli kukataza Wenye Ujauzito Warudi shuleni-Askofu
Na Jonas Kamaleki- MAELEZO
Katazo la Rais John Pombe Magufuli juu wasichana wanao pata ujauzito wakiwa shuleni kutoendelea na masomo ni sahihi kwani linalenga kurudisha maadili na heshima kwa wanawake hivyo hapaswi kushambuliwa kwa mitazamo hasi baadala yake mashambulizi hayo yaelekezwe kuimarisha mikakati ya kila kijiji wilaya na mikoa ya kumlinda mtoto wa kike na vitendo vya ubakaji.
Kwa kufanya hivyo wanafunzi watapata ulinzi wa kudumu kuanzia shule za awali msingi na sekondari dhidi ya vitendo viovu.
Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili,Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini zote Nchini, Askofu William Mwamalanga wakati akifunga kongamano la siku mbili lililoshirikisha vijana 2783 kutoka wilaya za Tanzania Bara ambao ni wajumbe wa kueneza Maadili na Amani vijijini kupitia mpango maalumu wa kuwafikia vijana kujiepusha na maadili hatarishi ya matumizi ya dawa za kulevya na kupinga elimu ya ugaidi kwa vijana wote nchini.
Askofu Mwamanga ambaye amekuwa kwenye mtandao wa kusaidia vijana nchini kwa miaka 16 ameitaja kauli ya Rais Magufuli kuwa ni kauli ya ukombozi kwa watoto wa kike na wazazi kwani hakuna mzazi anayempeleka mtoto shuleni kwenda kupata ujauzito.
“Kumshutumu Magufuli ni kitendo cha kulea majambazi wa umbakaji na ndoa za utotoni, hapa ni lazima Serikali iweke ulinzi kwa wanafunzi wa kike wanaosoma shule za mbali na makazi ikiwa ni pamoja na kuwapima wasichana wote wakati shule zinaanza kwa kila muhula wa masomo”, alisema Askofu Mwamalanga.
Mwenyekiti huyo amesema Rais Magufuli kwa hili yupo sahihi kwa asilimia 100 kwani dawa ya dhambi ni kuikata kwa macho meupe na siyo vinginevyo kuanzisha mijadala kwamba anawachukia wanawake siyo sahihi, Magufuli ana mke ana watoto kama tulivyo sote huyu ni mzazi tena Rais wa nchi anayejua tabu na shida pale mtoto wa kike anapobeba mimba na kukatizwa elimu. Kauli yake ina maana kwa wanafunzi kuzingatia elimu badala ya mapenzi,kwa watoto wa kike kuishikilia fursa ya elimu bure kwa nguvu kubwa na wenye kusimamia ulinzi kwao kuongeza mkakati huo zaidi na si vinginevyo.
Amewataka wakuu wa mikoa, wilaya, wakiwemo wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na miji kuisimamia kauli ya Rais Magufuli kwa vitendo kwa kuainisha maeneo hatarishi kwa wanafunzi wa kike ili wawe na ulinzi pamoja na kuanzisha ulinzi wa kuwafichua wabakaji kwa kila wilaya na kila kijiji baadala ya sasa ambapo watendaji hao wamegeuka kuwa wapongezaji wa kauli za Rais na wengine wakianzisha ibada feki za kumuombea Rais kazi ambayo haiwahusu kabisa kwani kazi ya maombi na dua ni yao viongozi wa kiroho.
Vijana hao kutoka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, Mashariki,Nyanda za Juu Kusini, Magharibi na Kanza ya Kusini, wamekiri kuwa ubakaji ni janga la kitaifa kwa mikoa yote nchini jambo ambalo limefanya tatizo hilo kuanza kuzoeleka na baadhi ya wanafunzi wasiopenda elimu kama njia ya kukwepa masomo ili waolewe, alisema Askofu Mwamalanga.
Aidha, Askofu Mwamalanga amewaonya baadhi ya wanasiasa na wanaharakati kuacha mchezo wa kuchezea maisha ya wanawake baadala yake wawe na msimamo chanya wa kumsaidia mtoto wa kike.
Kuna wanasiasa siku za karibuni walikuwa wakitetea wanafunzi wa kike wakijifungua wawe wanarudi shuleni siku hizi wamegeuka na wanatetea marufuku ya mtoto huyo huyo kutorudi shuleni watu wa namna hii hawafai kumsaidia msichana wa kizazi cha leo, ameonya Askofu huyo.
Vijana kutoka wilaya za Kyela, Ileje, Simiyu, Hai, Moshi, Songea, Liwale, Masasi, Lindi Morogoro, Dodoma, Nzega, Morogoro, Tabora, Chunya na Mbozi wamekiri kuwa wazazi wengi kwenye wilaya hizo ndiyo kikwazo kikubwa kwa wanafunzi kupata mimba wakiwa shuleni kutokana na wazazi au walezi hao kupokea mahari wakati mtoto akiwa shuleni, hivyo katazo la Rais Magufuli litaokoa wasichana wengi kama siyo wote.
Askofu Mwamalanga aliongeza kuwa baadhi ya vijana hao ambao ni walimu wa shule za msingi kutoka wilaya za Mtwara,Lindi, Tunduru, Mbinga, Makete, Ukerewe Mpanda, Kasulu,Tarime, Geita, Bukoba, Tabora, Kaliua, Momba, Dodoma Vijijini wameonya kuwa ili kumaliza tatizo la mimba shuleni ni lazima katazo la Rais lisimamiwe na wizara ya Elimu, Halimashauri za wilaya, madiwani na wenyeviti wa vijiji kwa kuwashirikisha walimu na wazazi kazi ambayo ni muhimu na huko ndiko kumpongeza Rais.
Naye Shekhe Kassimu Rajabu amewahimiza vijana hao kwenda kuyatendea kazi yote waliyojifunza kwenye kongamano hilo la aina yake ambalo limewashirikisha vijana wa dini mbali mbali nchini.
“Twendeni tukawe wajumbe mkoani mwetu ili kuibadilisha jamii ya vijana kutoka kwenye uhalifu mbalimbali ukiwemo ugaidi ambao unawanyemelea sana vijina na kuashiria uvunjifu wa amani”, alisema Shekhe Rajabu
Hivi karibuni akizindua Barabara ya Bagamoyo- Msata, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipiga marufuku wanafunzi wa kike kurudi shuleni baada ya kupata ujauzito. Kauli ya Mhe. Rais imeungwa mkono na watu wenye maadili na kupingwa na wanaharakati hasa asasi za kiraia.
Hivyo makala Msimshambulie Magufuli kukataza Wenye Ujauzito Warudi shuleni-Askofu
yaani makala yote Msimshambulie Magufuli kukataza Wenye Ujauzito Warudi shuleni-Askofu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Msimshambulie Magufuli kukataza Wenye Ujauzito Warudi shuleni-Askofu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/msimshambulie-magufuli-kukataza-wenye.html
0 Response to "Msimshambulie Magufuli kukataza Wenye Ujauzito Warudi shuleni-Askofu"
Post a Comment