Loading...
Loading...
- Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa , tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title :
link :

soma pia




Na. Othman Khamis. OMPR. 
Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } inakusudia kujenga Nyumba  Mpya  za Kisasa za Makaazi  katika Wilaya tofauti za Zanzibar kwa  ajili ya  Wananchi ambao Nyumba zao zimekumbwa na Maafa wakati wa msimu wa Mvua za Masika uliopita.

Ujenzi wa nyumba hizo unafuatia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  wa kuzitaka Nchi, Taasisi na Mashirika rafiki  ndani na nje ya Nchi kusaidia kuunga mkono Wananchi walioathirika na Mvua hizo ambao wengine wamepoteza kabisa Makaazi yao.

Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Bwana Said Al – Khemeir alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Said alisema Uongozi wa Taasisi yake ulifika Zanzibar kuangalia maeneo yaliyoathirika na Mvua hizo na kuandaa Mipango itakayosaidia kuanzwa kwa Mradi huo mkubwa utakaohusisha Wilaya zote zilizopatwa maafa hayo.

Alisema Awamu ya kwanza ya mradi huo itaanza Kisiwani Pemba kwa ujenzi wa Nyumba 30, zitakazokuwa na uwezo wa kuchukuwa Familia Mbili, Skuli yenye Madarasa Saba na Maktaba yake, Hospitali, Msikiti pamoja na Maduka kwa ajili ya wakaazi watakaoishi eneo husika.

Mwakilishi huyo  wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Emirates Red Crecent alisema Taasisi hiyo yenye kufanya kazi chini ya ushauri wa Vyama vya Msalaba  Mwekundu na Mwezi Mwekundu Duniani imekuwa ikitoa huduma za kibinaadamu katika Mataifa mbali mbali Duniani kutegemea na mahitaji ya Nchi husika.

Naye Mhandisi Muandamizi wa Taasisi hiyo ya Emirates Red Crecent Fateh Basel aliishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba maeneo yatakayotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba hizo ni vyema yakawa salama.

Mhandisi Basel alisema maeneo yatakayotengwa endapo yatakuwa  karibu na miundombinu ya Bara bara, Maji na Huduma za Umeme yatasaidia kurahisisha mradi huo kukamilika kwa haraka ili kutoa faraja kwa Wananchi waliothirika na Mvua za masika zilizopita.

Aliupongeza ushirikiano wa karibu ulioonyeshwa na watendaji wa Wilaya na Mikoa wakati wa ziara yao ya kukagua sehemu zilizoathirika na Mvua za Masika pamoja na kuangalia baadhi ya maeneo salama yenye sifa na haiba ya kujengwa kwa mradi huo.

Akitoa shukrani zake  kwa Uongozi wa Taasisi hiyo ya Emirates Red Crecent Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kitendo kilichobuniwa na Taasisi hiyo hakitolea faraja kwa Wananchi walioathirika na janga hilo pekee bali hata na Serikali Kuu kwa ujumla.

Balozi Seif alisema atauagiza Uongozi wa Kila Mkoa na Wilaya Visiwani Zanzibar kufanya utafiti na  uhakiki wa kuangalia maeneo yatakayoweza kuanzishwa miradi hiyo itakayostawisha Wananchi waliokusudiwa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi huo wa Emirates Red Scecent kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itazingatia wazo hilo kwa ajili ya kulitolea baraka zake ili Mradi huo uanze mara moja na kulet tija iliyokusudiwa.



Hivyo makala

yaani makala yote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/na_22.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to " "

Post a Comment

Loading...