Loading...
title :
link :
Na. Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametoa wito kwa Wazazi Nchini kuwahamasisha Vijana kujiunga na Skauti ili iwasaidie kuondokana na vijiwe ambavyo mara nyingi huwa ni mazalio ya vitendo vya kihuni visivyo hitajika katika Jamii na Taifa kwa ujumla.
Alisema Skauti ni Umoja ambao humjenga Kijana kuwa na tabia nzuri,ujasiri, uadilifu, uzalendo na kumfanya Kijana huyo huyo kuweza kukabiliana na mitihani yake ya kimaisha.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizifunga sherehe za Miaka 100 ya Skauti Tanzania zilizofanyika katika Kampas ya Chuo Kikuu Mjini Dodoma sherehe zilizotanguliwa na Wiki ya maonyesho ya kazi mbali zinazotekelezwa na Vijana wa Skauti Nchini.
Aliwataka Vijana waendelee kuulinda Umoja wao kwa gharama zozote utakaowavusha tena Miaka mengine Mia Moja ijayo ili wajenge Skauti yenye nguvu na inayoheshimika ndani ya Nchi na nje ya mipata ya Taifa la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi Seif alisema katika kipindi hicho Vijana wa Skauti wamepambana
na changamoto nyingi zilizotishia kuhatarisha ustawi wao lakini bado
wako imara uliotokana na ushirikiano na mshikamano wao vyenginevyo
wangekuwa wameshasambaratika.
Alisema Watanzania wamekuwa wakithaminiwa na kuwa na hadhi Duniani
kote kwa kuwa na Tunu ya Amani ambayo Nchi nyingi zinatamani kuwa na
Tunu kama hiyo huku zikiendelea kuitafuta kupitia njia mbali mbali
bila ya mafanikio yoyote yale.
Balozi Seif alifahamisha wazi kwamba kukosekana kwa amani hakuna
maendeleo isipokuwa vurugu, wasi wasi, chuki , visasi maradhi, njaa,
ukimbizi,uharibifu kwa Nchi, Wananchi na Mali zao na huchukuwa Miaka
mingi kuirejesha Amani iliyopotea.
Akizungumzia suala la Elimu, Balozi Seif alisema kwa kuwa asilimia
kubwa ya Vijana wa Skauti ni Wanafuzi waliwaasa kutoacha masomo yao
ya kila siku maskulini.
Aliwataka wasome kwa bidii na kuwa mfano mwema kwa Jamii ili wale
wanaoamini kujiunga na Skauti ni kupoteza muda na njia ya kumfanya
mwanafunzi asifaulu masomo yake , basi kauli hiyo ifutike katika fikra
zao zilizokuwa finyu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Chama cha
Skauti Tanzania kwa uamuzi wake wa kutoa Tuzo Maalum kwa Marais
Wastaafu pamoja na Watu waliofanya ushujaa na kuonyesha Uzalendo
katika Ujenzi wa Taifa hili.
Balozi Seif alisema kitendo cha kuwakumbusha Marasia hao wastaafu
inaashiria ni kiasi gani mchango wao umethaminiwa katika jitihada zao
za kukiendesha Chama cha Skauti Nchini Tanzania.
Alisema kwa nioaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar alitoa
shukrani za dhati kwa Chama cha Skauti Tanzania kwa kuipa heshima
Zanzibar ya kuandaa Jamboree ya Mwaka 2019 na kuahidi kwamba heshima
iliyotolewa itaenziwa kwa kuandaliwa Jamboree ya aina yake.
Akitoa Taarifa ya Sherehe za Maadhimisho hayo ya kutimia Miaka 100 ya
Skauti Tanzania Rais wa Chama cha Skauti Tanzania ambae pia ni Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania Profesa Joyce Ndalichako
alisema sherehe hizo zilizoadhimishwa kwa siku Tisa zimeshuhudiwa na
Vijana wa Skauti kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Comoro na Jamuhuri ya
Kidemokrasi ya Congo {DRC}.
Profesa Ndalichako alisema Vijana wa skauti walipata mafunzo mbali
mbali kama mapambano dhidi ya rushwa, Dawa za Kulevya pamoja na
ukakamavu katika kuwajenga kizalendo, maadili pamoja na heshima.
Rais huyo wa Chama cha Skauti Tanzania alitoa wito kwa Vijana na
Wanafunzi walioshiriki maadhimisho hayo kuzingatia mambo waliyojifunza
pamoja na kuyapeleka kwa wenzao ili lengo la kuanzishwa Skauti Nchini
liweze kufanikiwa vyema.
Naye akitoa salamu katika maadhimisho hayo Rais wa Skauti Zanzibar
ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki
Pemba Juma alisema Wizara hiyo itahakikisha katika kuona Vijana wa
Skauti wanaendelea kukua katika maadili yanayotakiwa katika Jamii.
Waziri Riziki alisema ukuaji huo unaozingatia maadili ndio njia pekee
itakayohakikisha kwamba Taifa linaelekea kwenye mfumo unaokubalika
kiheshima, nidhamu pamoja na utiifu.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akikagua maonyesho mbali mbali ya Vijana wa Skauti kutoka Mikoa yote
ya Tanzania Bara na Zanzibar, kutoa Nishani mbali mbali, Tuzo pamoja
na vyeti vya shukrani.
Zaidi ya Vijana Elfu 4,500 wa Skauti kutoka Mikoa yote ya Tanzania
walikuwepo Mkoani Dodoma tokea Tarehe 21 Julai kwenye wiki ya
Maadhimisho hayo ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania na kushiriki katika
shughuli mbali mbali ikiwemo maonyesho.
Pia sherehe hizo zilishuhudiwa na Vijana wa Skauti kutoka Mataifa
Jirani na Rafiki ya Kenya, Uganda, Rwanda, Comoro pamoja na Jamuhuri
ya Kidemokrasia ya Congo {DRC}.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/na_28.html
0 Response to " "
Post a Comment