Loading...
title : RAIS DKT MAGUFULI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50
link : RAIS DKT MAGUFULI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50
RAIS DKT MAGUFULI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50
RAIS Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo asimamishwe kazi kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.
Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Julai 28, 2017), na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.
Amesema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. “Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.”
Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini “Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi kuivumilia.”
Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.
Hivyo makala RAIS DKT MAGUFULI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50
yaani makala yote RAIS DKT MAGUFULI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT MAGUFULI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/rais-dkt-magufuli-aagiza-kusimamishwa.html
0 Response to "RAIS DKT MAGUFULI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50"
Post a Comment