Loading...

NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI

Loading...
NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI
link : NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI

soma pia


NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa bima ya afya ya Mtoto 'Toto Kadi' leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa kiu yake katika sekta ya afya ni kuona kila mtu ana bima ya afya.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kadi ya Bima ya Afya kwa Mtoto ‘Toto Kadi’ , amesema kuwa taifa kuwa lina maendeleo linatokana na msingi wa afya  ambapo msingi huo unatokana  na kuwa watoto wanaopata huduma za afya kwa uhakika.

Amesema kuwa  gharama za kulipa matibabu katika ukuaji watoto na hali uchumi  ni kubwa lakini kuwepo kwa bima hiyo kutanya wazazi kuwa na  furaha wakati wote hata ikitokea ugonjwa bima ndio inamaliza matatizo.
Ummy amesema kuwa wakati  anaingia madarakani alikutana na Rais Dk. John Pombe  Magufuli  alichoendanacho ilikuwa ni kuongeza ghrarama lakini Rais alisema hakuna kuongeza ghrama yeyote cha msingi waangalie jinsi ya kusaidia watanzania kuwa na bima.

Aidha Waziri  Ummy amewaomba Mfuko wa  Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  kuja na bima ya mama mjamzito itakayotumika wakati ujauzito na badaa ya kujifungua.

Ummy amesema kuwa kampeni hiyo iwe endelevu kwa nchi nzima ili watoto wote kuwa na bima ya afya hapo tutakuwa tunajenga taifa lenye msingi bora wa afya.Waziri  huyo ameitaka kuweka utaratibu wa kubandika mabango katika kila kumbi za starehe ili wanavyotumia vinywaji waweze kuangalia watoto kama wana kadi ya afya bima ya afya.

Nae Mwenyekiti wa Bodi NHIF, Anne Makinda amesema kuwa wanafanya kazi nguvu kuhakikisha watanzania wanapata huduma za afya  pamoja na kulipa watu wanaotoa huduma kwa bima ya afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiangalia muundo wa kadi ya bima ya afya ya Mtoto mara baada ya kuzindua leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipeana Mkono na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda  mara baada ya kuzindua bima  kadi ya bima ya afya kwa watoto leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi wa bima ya afya kwa mtoto katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga akizungumza juu ya mpango wa bima ya afya ya Mtoto katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza juu ya bima ya afya kwa mtoto katika jiji la Dar es Salaam wakati uzinduzi wa bima hiyo katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


Hivyo makala NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI

yaani makala yote NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/nhif-yazindua-mpango-wa-toto-afya-kadi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NHIF YAZINDUA MPANGO WA TOTO AFYA KADI"

Post a Comment

Loading...