Loading...
title : SADC Kuendelea Kusimamia Amani Katika Nchi Wanachama
link : SADC Kuendelea Kusimamia Amani Katika Nchi Wanachama
SADC Kuendelea Kusimamia Amani Katika Nchi Wanachama
Mwambawahabari
Na. Bushiri MatendaSerikali ya Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhakikisha kunakuwa na amani na mshikamano miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Akizungumza wakati akifungua mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Jumuiya hiyo leo Jijijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga alisema kuwa Tanzania itaendeleza jitihada zinazofanywa na SADC kwa nchi wanachama katika kuendelea kuimarisha Ushirikianao katika Siasa, Ulinzi na Usalama.
“Nawasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wetu wa SADC ambaye anaamini kuwa mkutano huu unatuleta pamoja katika kujenga ushirikiano wetu zaidi kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa na amani, umoja, mshikamano na ustawi kati ya nchi wanachama,” alisisitiza Dkt. Mahiga
Dkt. Mahiga alisema kuwa nchi wanachama zimeendelea kuwa eneo lenye usalama na ustawi kwa kuzingatia hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na umoja huo kupitia kamati mbalimbali zilizoundwa kushughulikia mageuzi katika nchi za Lesotho hali iliyosaidia Taifa hilo kufanya uchaguzi wa wabunge mwezi June 2017 kwa amani.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dr. Stergomena Tax akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa 19 wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya hiyo inayojadili ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama mapema hii leo Jijini Dar es SalaamA.
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (hawapo pichani) wakati akifungua mkutano wa 19 wa Kamati hiyo unaojadili ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama mapema hii leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa 19 wa Kamati hiyo unaojadili ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama mapema hii leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO)
Hivyo makala SADC Kuendelea Kusimamia Amani Katika Nchi Wanachama
yaani makala yote SADC Kuendelea Kusimamia Amani Katika Nchi Wanachama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SADC Kuendelea Kusimamia Amani Katika Nchi Wanachama mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/sadc-kuendelea-kusimamia-amani-katika_20.html
0 Response to "SADC Kuendelea Kusimamia Amani Katika Nchi Wanachama"
Post a Comment