Loading...

SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI

Loading...
SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI
link : SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI

soma pia


SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameunda kamati itakayo shirikisha wakuu wa mikoa yote Tanzania,  kwa Viwanda vyote vilivyobinafsishwa kuvitembelea na kuvikagua na kutoa taarifa ya maamuzi kwa viwanda vitakavyokuwa havifanyi kazi kwa kutokutii agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mkoani Pwani katika ziara yake ya kutembelea na kuzindua viwanda.

Waziri Mwijage ameyasema hayo leo ofisini kwake alipo kukutana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ambapo alisema adhma ya serikali ni kuhakikisha viwanda vinalindwa na kuongeza uzalishaji lakini pia serikali imejikita zaidi katika kuwasaidia wananchi kupata ajira katika viwanda.

Aliongeza kuwa, wengi walipenda kuanzisha viwanda kwa bei rahisi sana lakini wameshindwa kuviendeleza na wengine kufanya shughuli tofauti na iliyokusudiwa, Waziri amesema kamati hii itakaa Dar es salaam ambapo itashirikisha wataalamu kutoka idara mbalimbali za serikali na kupitia Viwanda vyote ili kuvikagua na kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi.

Pamoja na hilo la ubinafsishaji, Mwijage amezungumzia swala la Mchele wa bandia ambapo taarifa zimekuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Tanzania tunazalisha mchele bandia,  na kusema kuwa Tanzania hakuna mchele bandia na taarifa hizi ambazo zimekuwa zikisambaa zinaharibu jina la nchi yetu kwani sisi ni wazalishaji na wasambaji wakubwa wa mchele kwa nchini mbalimbali.

Waziri ameahidi kufanya ufuatiliaji muda wote na atakapopatiwa taarifa zozote kuhusiana na upatikanaji wa mchele bandia kwa kuomba kupigiwa simu kupitia no. 0800110827.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo.
Wanahabari wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


Hivyo makala SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI

yaani makala yote SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/serikali-kuunda-kamati-ya-kukagua.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI"

Post a Comment

Loading...