Loading...
title : TANAPA YAMPATIA DKT. JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA
link : TANAPA YAMPATIA DKT. JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA
TANAPA YAMPATIA DKT. JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA
Na Richard Mwaikenda
Dkt. Jane Goodal ambaye ni raia wa Uingereza alianza utafiti katika Hifadhi ya Gombe mnamo miaka ya 60 akiwa na umri wa miaka 26.
Katika utafiti wake amegundua mambo mengi ikiwemo jinsi Sokwe wanavyojitambua, kuwa na hisia na jinsi wanavyoishi kwa ushirikiano kama walivyo binadamu.
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt Goodal anasema wakati anaanza kufanya utafiti ilikuwa vigumu Sokwe hao kumkaribia kwani walikuwa wanamuogopa na ilikuwa ni mara ya kwanza kwao kumuona mtu mweupe, lakini alifanya jitihada hadi wakamzoea na kuanza kumsogelea na kumuona mtu wao wa karibu.
Anasema alitumia mbinu mbalimbali kama vile kuwapatia ndizi na vyakula vingine hadi wakamzoea.
Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Utalii katikati ya jiji la Dar es Salaam, viongozi na wageni waalikwa walipata wasaa wa kuangalia picha mbalimbali za matukio ya sokwe wakiwa na Jane Goodall.
Katika utafiti wake amefanikiwa kuanzisha chuo na kutunga vitabu pamoja na video zinazoelezea maisha yake na Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma.
Katika hafla hiyo walihudhuria Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara, Mwanasiasa Mkongwe Getrude Mongela, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Goodall, Mhe. Lembeli pamoja na mabalozi mbalimbali na waalikwa wengine. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi Dk. Jane Goodall tuzo maalumu kwa kutambua mchango wake wa utafiti wa miaka 60 wa maisha ya Sokwe pamoja na uhifadhi wa wanyama wengine kwenye hifadhi ya Gombe, mkoani Kigoma katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Tuzo hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa). Habari zaidi zitaletwa punde. (NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Dk. Jane Goodall akikabidhiwa cheti cha kutambua mchango wake kwa Tanzania kwa kuhifadhi Sokwe na wanayama wengine |
Dkt. Jane Goodall akipatiwa pia zawadi ya kinyago cha Sokwe
Dkt. Jane Goodall akikabidhiwa picha ya Sokwe
Mama Mongela akimvisha Dkt. Jane Goodall zawadi ya vitenge.
Hivyo makala TANAPA YAMPATIA DKT. JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA
yaani makala yote TANAPA YAMPATIA DKT. JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANAPA YAMPATIA DKT. JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/tanapa-yampatia-dkt-jane-goodall-tuzo.html
0 Response to "TANAPA YAMPATIA DKT. JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA"
Post a Comment