Loading...

WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA

Loading...
WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA
link : WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA

soma pia


WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA


Waajiri nchini wametakiwa kufanya uhakiki wa kina wa vyeti vya elimu kwa ajira mpya zitakazotolewa ili kuwa na watumishi wa umma wenye sifa zinazostahili katika utumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya  Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema uhakiki wa kina utasaidia sana kuepukana na kutojirudia tena kwa suala la watumishi wa umma wanaoghushi vyeti.
 “Jana tumetoa vibali vya ajira 10,184 kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, hivyo napenda niwasisitize sana waajiri wote kufanya uhakiki wa kina ili tusiwe tena na watumishi wa umma wasiostahili katika orodha ya malipo” Mhe. Kairuki amesema.

Waziri Kairuki amesisitiza kuwa zoezi la uhakiki ni endelevu ambapo lazima lifanyika pale mtumishi wa umma atakaporudi katika kituo cha kazi kutoka masomoni, na watakaorejea katika utumishi wa umma  baada ya likizo bila malipo au sababu nyingine.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Kinondoni (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya  kikazi katika wilaya hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally S. Happi akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Kinondoni leo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Wilaya hiyo kuzungumza na Watumishi wa Umma,  Jijini Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Bibi. Sixtha Kevin Komba akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi  kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Ukuzaji Maadili Ofisi ya Rais- Utumishi Bi. Leyla Mavika akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya maadili katika Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.

Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) baada ya kupokea hoja za watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam. Pichani- Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb)  na kushoto ni Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli. Picha na: Genofeva Matemu - MAELEZO.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA

yaani makala yote WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/waajiri-nchini-watakiwa-kufanya-uhakiki.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA KINA KWA AJIRA MPYA ZITAKAZOTOLEWA"

Post a Comment

Loading...