Loading...
title : TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI.
link : TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI.
TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI.
UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Everton kutoka nchini Uingereza imeridhishwa na huduma inayotolewa kwa wagonjwa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo mabusha na matende hapa nchini.
Hayo yamezungumzwa na mmoja wa viongozi wa Everton Bw. Darren Griffiths ambao ni washiriki katika kuchangia huduma ya magonjwa hayo hapa nchini ambaye ameongozana na timu yake ili kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Gor Mahia kutoka chini Kenya.
“Tunayo furaha kuona wagonjwa wengi waliokuwa wanaumwa mabusha na metende nchini Tanzania kwa sasa wamepona kabisa na tunahaidi kuwa na Wizara ya afya bega kwa bega katika kutokomeza magonjwa haya” alisema Bw. Darren Griffiths
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt. Vida Mmbaga amesema kuwa kutokana na ushiriki wa Everton katika kuchangia utoaji wa Huduma ya kutibu ugonjwa huo wamefanikiwa kupata ujuzi wa upasuaji hasa kwa wagonjwa wa mabusha na matende hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Vida Mmbaga akisisitiza juu ya baadhi ya juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya viongozi kutoka timu ya Everton na mwakilishi kutoka Liverpool katika zoezi lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
Mratibu wa Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akibadilishana Mawazo na Mwakilishi kutoka Liverpool wakati wa tukio la kusaidia waliokuwa wagonjwa wa mabusha na matende liliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mmoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza na aliekuwa mchezaji wa timu hiyo Leon Osman akigawa zawadi kwa waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi lakuwasaidia lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
Picha ya pamoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza, Viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi lakuwasaidia lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Hivyo makala TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI.
yaani makala yote TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/timu-ya-everton-yaridhishwa-na-utoaji.html
0 Response to "TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI."
Post a Comment