Loading...
title : WANAWAKE WAPONGEZA MWENGE WA UHURU KUWAEPUSHA KUCHANGIA MAJI NA MIFUGO
link : WANAWAKE WAPONGEZA MWENGE WA UHURU KUWAEPUSHA KUCHANGIA MAJI NA MIFUGO
WANAWAKE WAPONGEZA MWENGE WA UHURU KUWAEPUSHA KUCHANGIA MAJI NA MIFUGO
Wanawake wa Vijiji vya Merya na Ikugha katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida wameushukuru Mwenge wa Uhuru kwa kuwafungulia mradi ambao umewaepusha kutembea umbali mrefu kutafuta maji ya kutumia ambayo si safi wala salama huku wakiyachangia na mifugo yao.
Wanawake hao wametoa pongezi hizo mara baada ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour kufungua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 49 utakaohudumia vijiji hivyo ambao umegharimiwa na shirika la saving International, halmashauri ya Singida pamoja na michango ya wananchi.
Wamesema kabla ya kupatikana mradi huo wanawake wa vijiji hivyo wamekuwa wakifuata maji umbali mrefu sana kiasi cha kushindwa kutekeleza shughuli nyingine za kuzalisha mali.
“Tulikua tunatembea mpaka tunachoka, tunaamua kupumzika njiani kwanza ndio tuendelee na safari ya kuleta maji nyumbani, yani tunashukuru sana kwakweli”, ameongea Bi Greta Senge Mkazi wa kijiji cha Ikugha.
Aidha wameongeza kuwa mradi huo utawapatia maji safi na salama kwakuwa maji waliyokuwa wakiyafuata umbali mrefu hapo awali yalikuwa machafu na si salama.
“Yani tulikuwa tunachota maji ambayo unakuta ng’ombe anakunywa hapohapo, wakati mwingine anajisaidia na inabidi uchote hivyo hivyo, kwakweli tunaushukuru sana mwenge kutufungulia mradi huu, tulikua tunaumwa matumbo kila mara”, ameongeza Rehema Lazaro.
Wameongeza kuwa mradi huo utapunguza magonjwa ya tumbo na macho ambayo yamekuwa yakiwasumbua mara kwa mara hukua wakiridhia kulipia kiasi cha shilingi 50 kwa lita 20 za maji ili kupata fedha za kutunza mradi huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akimtwisha ndoo ya maji moja ya akina mama waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Merya Wilayani Singida.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akifungua maji katika bomba wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Merya Wilayani Singida, pembeni yake Mkimbiza Mwenge Kitaifa Fredrick Ndahani.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akitazama vitunguu katika shamba la mboga mboga la umwagiliaji kwa njia ya matone wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Msange Wilayani Singida.
Sehemu ya shamba la mbogamboga lenye kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone ambapo vitunguu vinaonekana vimestawi vizuri, shamba hilo lina ukubwa wa ekari 25.

Hivyo makala WANAWAKE WAPONGEZA MWENGE WA UHURU KUWAEPUSHA KUCHANGIA MAJI NA MIFUGO
yaani makala yote WANAWAKE WAPONGEZA MWENGE WA UHURU KUWAEPUSHA KUCHANGIA MAJI NA MIFUGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAWAKE WAPONGEZA MWENGE WA UHURU KUWAEPUSHA KUCHANGIA MAJI NA MIFUGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/wanawake-wapongeza-mwenge-wa-uhuru.html
0 Response to "WANAWAKE WAPONGEZA MWENGE WA UHURU KUWAEPUSHA KUCHANGIA MAJI NA MIFUGO"
Post a Comment