Loading...
title : BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA
link : BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA
BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA
Na Lawrence Raphaely - Bunge.
Balozi wa China nchini LU Youqing amefika Ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai Jijini Dar es Salaam mapema leo kumuaga baada ya muda wake wa kukaa Tanzania kwisha.
Akizungumza na Spika Ndugai, Balozi huyo alisema kuwa muda wake wa kutumikia kama Balozi wa China hapa nchini umekwisha hivyo hana budi kuondoka ingawa angetamani kuendelea kubaki.Balozi huyo aliongeza kuwa amefurahi kuona kuwa katika kipindi chake chote akiwa hapa nchini uhusiano baina ya Tanzania na China umezidi kukua.
“Ninafuraha kubwa wakati ninaporejea China kuona kuwa uhusiano wetu wa kihistoria umezidi kukua na kwamba kuna ongezeko kubwa la uwekezaji wa China hapa Tanzania na pia tumesaidia katika utekelezaji wa miradi mingi,” alieleza Balozi huyo.
Balozi huyo ambaye amesema kuwa Tanzania ni nchi yake ya mwisho kuhudumu kama Balozi aliongeza kuwa kwa sasa anarejea nchini China na akiwa huko ataendelea kujitikita katika shughuli za kudumisha uhusiano baina ya Tanzania na China.
“Tanzania ndiyo nchi yangu ya mwisho kuhudumu kama Balozi na nitakaporejea nyumbani (China) nitaendelea kufanya shughuli nyingine ambazo zinalenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na China,” alisema Balozi Youqing.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Balozi wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake akimueleza jambo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimkabidhi zawadi Balozi wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA
yaani makala yote BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/balozi-wa-china-afika-ofisini-kwa-spika.html
0 Response to "BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA"
Post a Comment