Loading...
title : DC AWAALIKA WANAKE WA DSM KWENYE JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, LITAKALO ZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN.
link : DC AWAALIKA WANAKE WA DSM KWENYE JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, LITAKALO ZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN.
DC AWAALIKA WANAKE WA DSM KWENYE JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, LITAKALO ZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN.
Mkuu wa wilaya ya ilala Bi sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari Hawapo kwenye picha siku ya leo kutoa taarifa rasmi za ufunguzi wa jukwaa la uwezeshwaji kiuchumi kwa wanawake( Picha zote na John Luhende )
Makamu wa rais wa jJamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduziwa jukwaa la uwezeshwaji kiuchumi wanawake mkoa wa Dar es salaam , jukwaa ambalo limeandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanawake wa hali ya chini.
Baadhi ya wanahabari wakiendelea na majukumu yao ya kuchukua taarifa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya ilala .
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Ilala mhe. Sophia Mjema amesema kuwa jukwaa hilolitasaidia wanawake ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuendeleza biashara zao ambapo takribani zaidi ya wanawake elfu tatu 3000 kutoka wilaya zote jijini Dar wanatarajiwa kushiriki jukwaa huilo.
Mjema ameongeza kuwa uzinduzi huo utafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 26/08/2017 kuanzia majira ya saa tatu kamili asubuhi huku akitaja eneo husika litakalo fanyika tukio hilo kuwa ni maeneo ya viwanja vya Posta kijitonyama kama unaelekea makumbusho ukiwa umetokea mjini posta barabara ya Bagamoyo
Akifafanua zaidi juu ya uzinduzi wa Jukwaa hilo amesema kuwa Makamu wa Rais alizindua jukwaa hilo kwa mara ya kwanza na alilizindulia katika mkoa wa Dar es salaam na baadae akatoa maagizo kwa jukwaa hilo kuanzishwa na kuboreshwa kwa ngazi za kila Mikoa,Wilaya,tarafa,kata hadi mtaa .
'Napenda kutoa wito kwa wanawake pamoja kina mama wote kujitokeza kwa wingi ndio maana nasema Wanawake jitokezeni kwa wingi Jumamosi tujumuike sote na makamu wa rais kwa ajili ya Uzinduzi wa jukwaa letu litakalotukomboa kiuchumi.' Alisema Dc Mjema
Katibu Mtendaji wa baraza la uwezeshaji kitaifa (NEEC)Beng'i Issa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwa mkuu wa wilaya ya ilala kwa ajili ya kuzungumzia katika uzinduzi wa jukwaa la akina mama la uwezeshwaji kiuchumi litakalofanyika siku ya jumamosi.
Naye Katibu Mtendaji baraza la Taifa la uwezeshaji kiuchumi , Beng'i Issa Amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni katika kuwaunganisha akina mama katika kuwasidia kupata mitaji,mikopo,mafunzo nk.
Pamoja na hayo ametoa wito kwa akina mama wote wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya uzinduzi wa jukwaa hilo kwa akina mama wote wale wa kipato cha chini cha kati,na cha juu kuanzia akina mama ntilie na wafanyabiashara wadogo wadogo ili kupata kutambua mambo mengi yatakayo wasaidia kutambua pamoja na kukuzwa kifikra na uchumi pia .
Hivyo makala DC AWAALIKA WANAKE WA DSM KWENYE JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, LITAKALO ZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN.
yaani makala yote DC AWAALIKA WANAKE WA DSM KWENYE JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, LITAKALO ZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC AWAALIKA WANAKE WA DSM KWENYE JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, LITAKALO ZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/dc-awaalika-wanake-wa-dsm-kwenye-jukwaa.html
0 Response to "DC AWAALIKA WANAKE WA DSM KWENYE JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, LITAKALO ZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN."
Post a Comment