Loading...
title : MAKONDA: ASKARI POLISI WASIO WADILIFU WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA .
link : MAKONDA: ASKARI POLISI WASIO WADILIFU WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA .
MAKONDA: ASKARI POLISI WASIO WADILIFU WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA .
Mwambawahabari
Makonda akiendesha moja ya pikipiki hizo.
Maria Kaira, Mwambahabari
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka askari wa jeshi la polisi, wasio waadilifu na wanaotumia sheria vibaya ya kuwakandamiza wananchi kuachana nayo Mara moja, kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha amani,pia amesema kuwa askari yoyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo achukulie hatua za kisheria .
Makonda ameyasema hayo leo hii wakati akikabidhiwa pikipiki 10 za traffic ,kutoka katika kampuni ya TONGBA, ambazo zitasaidia katika misafara ya viongozi na kwa wananchi wanaohitaji msaada wa kupeleka wagonjwa hospitali , ambapo amesema anasikitishwa na baadhi ya askari wanaotumia madaraka yao ya kuwanyanyasa wananchi na kuahatarisha usalama wa raia na mali zao kwa ujumla.
"Masikitiko yangu ni kuona baadhi ya askari kutokuwa waminifu,waadilifu,na wanaoweza kufanya kazi yao kijume na taratibu,kwani polisi wana haki ya kulinda na kuhakikisha sheria inafuatwa pamoja na kuwalinda wananchi, sitaki kuona askari wa jeshi la polisi wanaovunja sheria wala hakuna mtu atakaetumia magwanda yake na sheria za polisi kuwakandamiza wananchi wa mkoa wa Dar es salaam". Amesema Makonda.
Aidha Makonda amemtaka kaimu kamanda kanda maalumu ya Dar es salaam, kuhakikisha askari wote waliovunja sheria kukamatwa Mara moja na kuwekwa ndani kwa kosa la kutumia sheria vibaya,pia ameongeza kuwa katika kuimarisha ulizi na usalama atahakikisha kamera zinafungwa katika vituo vyote vya polisi ikiwa na lengo la kuimarisha usalama.
'' Natuma salama kwa jeshi la polisi hakuna mtu yoyote atakae endelea kutumia magwanda wala sheria ya kwa kuwa polisi kwa kuwakandamiza wananchi, polisi mpo kwa ajili ya kusimamia sheria na kualinda wananchi na mali zao pamoja na kupambana na uhalifu''
Pia kwa upande mwingine Makonda amewakabidhi walemavu wa miguu magongo yatakayoweza kuwasaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine ikiwa ni moja ya ahadi yake aliyotoa, kwa lengo la kuwafanya walemavu hao kujiona ni sawa na wananchi wengine.
Hata hivyo Mwambawahabari ulizungumza na mmoja wa walemavu hao Bi Rehema na kusema kuwa anamshukuru mkuu wa mkoa wa jiji la Dar es salaam kwa kuwasaidia kuwapa magongo, pia ameimba serikali kuwasaidia watu wenye ulewavu kuanzisha mfuko utakaowasaidia, ambao mfuko huo utakuwa chini ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda , akikabidhi magongo kwa walemavu waliotoka katika maeneo mbalimbali.
Hivyo makala MAKONDA: ASKARI POLISI WASIO WADILIFU WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA .
yaani makala yote MAKONDA: ASKARI POLISI WASIO WADILIFU WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA: ASKARI POLISI WASIO WADILIFU WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA . mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/makonda-askari-polisi-wasio-wadilifu.html
0 Response to "MAKONDA: ASKARI POLISI WASIO WADILIFU WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA ."
Post a Comment