Loading...
title : DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA
link : DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA
DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA
Na Fredy Mgunda,Iringa
Halmashauri ya wilaya ya kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka mingi katika mji mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha dola za kimarekani 9,548,827 kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji yatakayo weza kutatua changamoto hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa wameamua kutafuta chanzo kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa Ilula.
“Leo nimefika hadi huku kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa kitafanikiwa kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani ya chama na kuhakikisha kuwa wanatatua matatizo ya wananchi”alisema Masenza
Aidha Masenza alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania dr John Pombe Maguli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wake.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alivitaja baadhi ya vyanzo ya maji na uwezo wa uzalishaji ambavyo vinatoa huduma kwa mji mdogo wa Ilula ni Ilomba kutoka kijiji cha Imalutwa na Idemule kutoka kijiji cha Mazombe kwa ujumla vinazalisha wastani wa uzalishaji wa maji wa mita za ujazo 1,142 kwa siku.
Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula
Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula
Hivyo makala DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA
yaani makala yote DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/dola-milioni-95-kutatua-tatizo-la-maji_24.html
0 Response to "DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA"
Post a Comment