Loading...
title : Emmerson Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais wa Zimbabwe leo.
link : Emmerson Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais wa Zimbabwe leo.
Emmerson Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais wa Zimbabwe leo.
Mnangagwa aapishwa kuwa Rais wa Zimbabwe.
Emmerson Mnangagwa ameapishwa kuwa Rais wa Zimbabwe siku moja baada ya mshindani wake mkuu Nelson Chamisa kutangaza kukataa matokeo ya uchaguzi.
Mapema Jumapili waangalizi wa uchaguzi kutoka Marekani walisema nchi hiyo imekosa utamaduni wa uvumilivu wa demokrasia.
Siku ya Ijumaa mahakama ya kikatiba ilikataa madai ya upinzani kuwa udanganyifu ulifanyika ikisema kuwa hakukuwa na ushahidi.
Uchaguzi huo wa mwezi Julai ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa miaka mingi Robert Mugabe aondolewa madarakani mwaka uliopita.
Siku mbili baada ya uchaguzi huo watu 6 waliuawa kwenye ghasia kati ya jeshi na wafuasi wa muungano wa upinzani MDC, unaodai kuwa kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa alikuwa ameibiwa ushindi wake.
Saa kadhaa kabla ya Mnanganwa kuapishwa taasisi ya kiamataifa ya Marekani inayohusika na masuala ya Demokrasia ilisema mfumo wa Zimababwe haukuruhusu vyama vya kisiasa kutendewa kwa njia iliyo sawa na watu hawakuruhusiwa kupiga kura kwa njia huru.
Hivyo makala Emmerson Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais wa Zimbabwe leo.
yaani makala yote Emmerson Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais wa Zimbabwe leo. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Emmerson Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais wa Zimbabwe leo. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/emmerson-mnangagwa-aapishwa-kuwa-rais.html
0 Response to "Emmerson Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais wa Zimbabwe leo."
Post a Comment