Loading...

Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba

Loading...
Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba
link : Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba

soma pia


Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba

KUTOKANA na changamoto nyingi za ukosefu wa makazi ya kuaminika kwa watu wengi, mshindi wa Sh Milioni 20, Innocent Nyeriga, amesema anatafakari fedha zake alizokabidhiwa jana mjini Dodoma aziweke kwenye ujenzi wa nyumba.

Nyeriga mkazi wa Dodoma na mshindi wa Biko droo ya 29 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa fedha zake jana Jumatatu katika benki ya NMB, Mjini Dodoma tayari kwa kuanza kuzitumia kwa matumizi yake ya kawaida.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Nyeriga anayejighulisha na kibarua cha kuhudumia mifugo mjini Dodoma, alisema kwamba lengo lake haswa ni kujenga nyumba nzuri ili familia yake iondokane na changamoto ya ukosefu wa makazi bora.

“Nawashukuru Biko bahati nasibu iliyokomboa maisha yangu, hivyo fedha hizi tangu mwanzo nilizipanga nijengee nyumba saa chache baada ya kupewa taarifa ya ushindi wangu, nikiamini haya yote yameletwa na Mungu kwa kuwatumia Biko,” Alisema Nyeriga.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema mchezo wa Biko ni mzuri na rahisi kucheza pamoja na kushinda kwake, huku akiwataka Watanzania kuchangamkia ili waweze kuvuna mamilioni ya zawadi kwa kuanzia zile papo kwa hapo bila kusahau donge nono la Jumatano na Jumapili la Sh Milioni 20 kama alizonyakua Nyeriga.

“Mchezo huu wa Biko unachezwa kwa kutumia simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo wanachotakiwa ni kufanya miamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya Kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.

“Mbali na kushinda zawadi kubwa ya Sh Milioni 20 ambayo ni lazima iende kwa mshindi Jumatano na Jumapili, lakini pia zawadi za papo kwa hapo zinatoka kila dakika ambazo ni zile za Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja inayoenda kwa mshindi mara baada ya kupokea ujumbe wa ushindi kwenye simu anayotumia kuchezea Biko,” Alisema Melles.

Kwa kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Dodoma, mshindi mwingine wa Milioni 20 anatarajiwa kujulikana katika droo ya kesho Jumatano maarufu kama Jumatamu na nyingine itakuwa Jumapili huku ikiitwa Jumadili na waendeshaji hao wa Biko.
Mshindi wa Droo ya 29 ya Biko, Innocent Nyeriga wa pili kutoka kulia akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles wa pili kutoka kushoto mwenye fulana ya Biko.
Shughuli ya makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wa Dodoma, Innocent Nyeriga ikiendelea katika benki ya NMB jana mjini Dodoma.


Hivyo makala Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba

yaani makala yote Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/innocent-nyeriga-milioni-20-za-biko.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba"

Post a Comment

Loading...