Loading...
title : COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE
link : COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE
COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE
Na Dotto Mwaibale, Lindi
MAOFISA ugani mkoani Lindi wamesema wanashindwa kuwahudumia kikamilifu wakulima kutokana na kukosekana kwa usafiri wa kuwapeleka vijijini pamoja na kutelekezwa na wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kushindwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara.
Wakizungumza juzi katika mafunzo kuhusu kilimo bora yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, COSTECH, maofisa ugavi hao walisema kutokana na upungufu wa wataalam hao wamekuwa wanahudumia vijiji vingi na mtu mmoja anaweza kuhudumia vijiji hadi sita.
Pia walisema kwamba tatizo lignine wamekuwa hawapati mafunzo ambayo yatawezesha waweze kwenda na wakati.
Ofisa Ugani kutoka Manispaa ya Lindi Hussein Mwapili alisema wizara ya kilimo baada ya kuwakabidhi maafisa ugani kwa halmashauri imeshindwa hata kuwafuatilia na hata kuwajengea nyumba wakati wizara zingine kama elimu na afya zinawakumbuka wataalamu wao kwa kuwajenge nyumba na kuwapa miongozo ya mara kwa mara.
“Sisi tumesahulika kabisa, tunakumbukwa wakati wa njaa tu ndipo utaona tunalaumiwa kwamba tunaishi mjini, lakini wizara ya kilimo imefanya nini kuhakikisha maafisa ugani wanaishi katika mazingira bora ya kufanyia kazi? Kule vijiji tunaambiwa tukaishi huko je kuna nyumba za wagani? alihoji.
Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija kwa maofisa Ugani wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani hapa juzi.
Ofisa Kilimo kutoka Manispaa ya Lindi, Amina Pemba akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Maofisa Ugani wakipata mafunzo.
Hivyo makala COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE
yaani makala yote COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/costech-ilivyowanoa-maofisa-ugani-wa.html
0 Response to "COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE"
Post a Comment