Loading...
title : Lipumba atema cheche , kuhusu uhalali wa wabunge 8 aliowateua.
link : Lipumba atema cheche , kuhusu uhalali wa wabunge 8 aliowateua.
Lipumba atema cheche , kuhusu uhalali wa wabunge 8 aliowateua.
Mwambawahabari
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anaetambuliwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba amelitolea ufafanuzi suala la wabunge nane wa viti maalum walioteuliwa na chama chake hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anaetambuliwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba amelitolea ufafanuzi suala la wabunge nane wa viti maalum walioteuliwa na chama chake hivi karibuni.
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam Profesa Lipumba ameeleza kuwa wabunge hao wa viti maalum ameteuliwa kihalali kwa kufuata katiba ya CUF,ambapo amefafanua kuwa Julai 2015 CUF kupitia kikao cha baraza kuu ilipitisha majina wa wabunge wa viti maalum, ambapo tarehe 28 Septemba 2015 nakala hiyo ilisainiwa na katibu Mkuu Seif Sharif Hamad na kupelekwa ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Lipumba ameeleza kuwa anashangazwa na Katibu Mkuu wa CUF kufungua kesi ya kuvuliwa uanachama kwa wabunge nane kwa hati ya dharula wakati yeye ndiye aliye isaini hiyo barua na kuipeleka NEC.
Wabunge hao nane walivuliwa uanachama kwa makosa ya kukiuka katiba ya CUF kwa kukihujuma chama hicho.
Katika hatua nyingine ProfesaLipumba amemtaka Maalim Seif kurudi kazini ili waendelee kushirikiana kama zamani.
"Maalim analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni boss kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi hapa. Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia simu hapokei, nasikia saizi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze" Alisema Lipumba
Hivyo makala Lipumba atema cheche , kuhusu uhalali wa wabunge 8 aliowateua.
yaani makala yote Lipumba atema cheche , kuhusu uhalali wa wabunge 8 aliowateua. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Lipumba atema cheche , kuhusu uhalali wa wabunge 8 aliowateua. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/lipumba-atema-cheche-kuhusu-uhalali-wa.html
0 Response to "Lipumba atema cheche , kuhusu uhalali wa wabunge 8 aliowateua."
Post a Comment