Loading...

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI

Loading...
MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI
link : MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI

soma pia


MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaleo (Jumatano, Aprili, 25, 2018) ameshiriki maziko ya aliyekuwa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu marehemu Bw. Atufigwege Mwakasege yaliyofanyika katika makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma. 
Bw. Mwakasege ambaye alihamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 29, 2016 akitokea Ofisi ya Rais-TAMISEMI amefariki dunia Aprili 23 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema kifo hicho kimeiachia pengo kubwa  kwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na familia. 
“Natumia fursa hii kutoa pole kwa wanafamilia hususan mjane na watoto. Marehemu ameacha pengo ndani ya familia, hivyo tumuombe Mwenyezi Mungu awape uwezo na nguvu ya kuweza kuhimili pengo hilo.” 
Marehemu Bw. Mwakasege ambaye alizaliwa Desemba 25, 1959 katika kitongoji cha Mwanjelwa mkoani Mbeya, ameacha mjane Bibi Judith Mwakasege pamoja na watoto wane ambao ni Henry, Joel, Eva na Kelvin Mwakasege. 
Maziko hayo pia yamehudhuriwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mama Mary Majaliwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola, Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi, Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wakati huo huo, WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Bw. Abbas Kandoro ambaye amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu.
Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatano, Aprili 25, 2018), Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta Bw. Kandoro na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye hospitali hiyo wakihudumiwa vizuri. 
Pia Waziri Mkuu amemjulia hali Mbunge wa Viti Malumu (CUF) Bi. Shamsiha Azizi Mtambo ambaye amelazwa katika ya Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU)kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu. 
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku.
Kwa upande wake, Bw. Kandoro alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia hali, pia aliwashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali hiyokwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa mfanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Atufigegwe Mwakasege, nyumbani kwa marehemu eneo la Kikuyu mjini Dodoma Aprili 25, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  wakiweka shada la  maua kwenye kaburi la mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Atufigegwe Mwakasege katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro ambaye amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma kwa matibabu leo  Aprili 25, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu




Hivyo makala MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI

yaani makala yote MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/majaliwa-ashiriki-mazishi-ya-mtumishi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI"

Post a Comment

Loading...