Loading...
title : Mashindano ya BASEBALL Tanzania Kufanyika Zanzibar.
link : Mashindano ya BASEBALL Tanzania Kufanyika Zanzibar.
Mashindano ya BASEBALL Tanzania Kufanyika Zanzibar.
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Chama cha Baseball na Softball Zanzibar (ZABSA) kimeandaa Mashindano maalum ya Mabingwa ya mchezo huo Mashindano ambayo itashirikisha timu za Zanzibar na Tanzania Bara ambapo kesho Jumamosi yakitarajiwa kuanza na kumalizika kesho kutwa Jumapili katika viwanja vya Amaan Nje.
Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Chama hicho Othman Ali Msabaha amesema lengo la kuandaa Mashindano hayo ni kuzidi kuuhamasisha mchezo huo ambao kwa Zanzibar una miaka 3 wakati kwa bara una miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.
“Lengo la Mashindano haya ni kuzidi kuusambaza huu mchezo mana tunataka uzidi kukuwa kwa kasi sana, na pia tunataka uwe mpaka kwenye vikosi vya ulinzi na mitaani isiwe kwenye Mashule tu”. Alisema Msabaha.
Jumla ya timu 4 zitashiriki Mashindano hayo zikiwemo mbili kutoka Tanzania Bara timu ya Skuli ya Azania pamoja na Kibasila ambapo kwa Zanzibar zitashiriki timu za Skuli ya Mwanakwerekwe pamoja na Kombain ya Unguja.
Hivyo makala Mashindano ya BASEBALL Tanzania Kufanyika Zanzibar.
yaani makala yote Mashindano ya BASEBALL Tanzania Kufanyika Zanzibar. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mashindano ya BASEBALL Tanzania Kufanyika Zanzibar. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/mashindano-ya-baseball-tanzania.html
0 Response to "Mashindano ya BASEBALL Tanzania Kufanyika Zanzibar."
Post a Comment