Loading...

Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge

Loading...
Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge
link : Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge

soma pia


Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, mara baada ya kuwasili katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga kwa ajili ya kuanza ziara hiyo

Msimamizi wa Uzalishaji na Ujenzi katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Said Ngongoki akielezea jinsi uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara walipofanya ziara kiwandani hapo

Meneja Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa ( wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akibadilishana mawazo na mwakilishi kutoka Idara ya Biashara katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Emily Wu (kulia) katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.
Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Dominick Ngunyali (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya jinsi gesi inavyopokelewa katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la kupokelea gesi hiyo

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

Meneja Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa (kushoto) akielezea jinsi udongo wa aina mbalimbali unavyochanganywa katika hatua za awali za maandalizi ya utengenezaji wa vigae (tiles) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Mitambo katika Kituo za Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi cha Somangafungu kilichopo mkoani Lindi, Edwin Konyani katika ziara hiyo.

Msimamizi wa Bomba la Gesi Upande wa Umeme katika Kituo cha Kupokea Gesi kutoka Songosongo na Madimba Joseph Msafiri (katikati) akielezea jinsi gesi inavyopokelewa katika kituo hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika ziara hiyo.

Sehemu ya Kituo cha Kupokea Gesi kutoka Songosongo na Madimba kilichopo Somangafungu mkoani Lindi.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ameongoza Kamati y Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika maeneo mbalimbali yenye miradi ya gesi katika mkoa wa Lindi lengo likiwa ni kuona utekelezaji wa miradi hiyo.

Kati ya maeneo waliyotembelea ni pamoja na Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Somangafungu, Makutano ya Bomba la Gesi Asilia (Somangafungu) mkoani Lindi pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa Mitambo ya Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) lililoko katika Manispaa ya Lindi.


Hivyo makala Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge

yaani makala yote Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/matukio-dk-pallangyo-aongoza-kamati.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matukio : Dk. Pallangyo Aongoza kamati Bunge"

Post a Comment

Loading...