Loading...
title : MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO
link : MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO
MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO
MSHINDI Mkuu wa mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka , Rashid Ally, leo amekabidhiwa sh.milinoni 80 alizojishindia katika droo kubwa iliyochezwa Jumapili.
Rashid ambaye alijishindia kiasi hicho cha fedha katika mchezo huo wa Tatu Mzuka, alionyesha kutoamini, huku akiwa na furaha na shukrani baada ya ushindi huo wa kihistoria. Rashid, ambaye ana umri wa miaka 21 tu, anaishi na familia yake maeneo ya Temeke, Dar es Salaam.
Akizungumzia ushindi wake, Rashid ambaye amemaliza kidato cha nne hivi karibuni, alisema kuwa alikuwa anacheza angalau mara 4 hadi 6 kwa wiki kwa kutumia pesa aliyokuwa anaipata katika shughuli zake za kila siku.
'Ndoto yangu ni kujenga nyumba, na kuwekeza katika kilimo, kitu ambacho nitafanya kwa kushirikiana na mama pamoja na Baba yangu. Nia yangu ni kuikuza iwe ni biashara kubwa ' alisema Rashid.
Pia alisema ana mpango wa kuendelea kucheza mchezo na kuwa balozi wa Tatu Mzuka, ili kuwasaidia watu kufurahia mchezo huo na kuuamini. "Watu wengine ni wagumu kuamini kwamba unaweza kushinda kiwango hiki kikubwa cha fedha kupitia shilingi 500 tu. Ninafurahi kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuthibitisha hili"
Balozi wa Mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 80 Mshimdi Mkuu wa Mchezo huo, Rashid Ally katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Regence Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Lumuliko Mengele, akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni mama wa mshindi huyo, Fatma Kavila. Katikati ni mshindi, Rashid Ally.
Baba, mama na mwana wakiwa wameshika mfano wa hundi wa kiasi hicho cha fedha alichoshinda mtoto wao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO
yaani makala yote MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/mshindi-wa-mzuka-jackpot-akabidhiwa.html
0 Response to "MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO"
Post a Comment