Loading...
title : MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA DROO YA PILI YA “WEKA AKIBA NA USHINDE”
link : MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA DROO YA PILI YA “WEKA AKIBA NA USHINDE”
MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA DROO YA PILI YA “WEKA AKIBA NA USHINDE”
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.
BENKI ya Mawlimu, (Mwalimu Commercial Bank plc), imewakabidhi zawadi washindi watatu wa kampeni ya “weka akiba na ushinde’ ambapo mteja wa benki hiyo kutoka wilayani Newala, Bw.Khamisi Mmuka, alijinyakulia zawadi ya IPAD.
Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi iliyofanyika alasiri ya Agosti 7, 2017 kwenye tawi la Samora la benki hiyo, washindi wengine ni Bi.Flora Mbaule na Bi.Macrina Yoram Kyando wote kutoka Temeke jijini Dar es Salaam ambao walijnyakulia vocha za manunuzi.
Akizungumza kweney hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa alisema, kampeni hiyo ilianza Mei 18, 2017 ambapo mteja mwenye akaunti kila anapoweka akiba ya fedha kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) kwenyeakaunti yake, aliingia moja kwa moja kwenye droo hiyo. “Na sio mteja wetu tu hata mwananchi aliyefungua akaunti na kuweka kiasi kama hicho cha fedha naye pia alipata fursa ya kushiriki.” Alifafanua Bi. Rahma.
Naye Meneja wa tawi la Samora wa benki hiyo, Bi.Leticia Mmuka, alisema ingawa kampeni hiyo imemalizika lakini amewahimiza wananchi kufungua akaunti kwenye benki hiyo na wale wenye akaunti waendelee kuweka fedha zao kwani benki inatoa huduma bora na zenye kuvutia wateja.
Alisema huduma huizo ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni sukuhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali, wafanyabiashara, wakulima na wananchi kwa ujumla.
“Huduma za kibenki zitolewazo na MCB ni pamoja na mikopo yenye riba nafuu, huduma ya ATM iliyounganishwa na mtandao mpana wa UMOJA SWITCH uliosambaa nchi nzima.” Alifafanua zaidi.
Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole, (wapili kushoto), akimkabidhi zawadi ya IPAP, Bw. Khamisi Mmuka, kutoka wilayani Newala mkoani Mtwara, baada ya kuibuka mshindi kwenye droo ya kampeni ya "weka akiba na ushinde" iliyochezeshwa na benki hiyo. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa.
Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi la kutoa zawadi.
Hivyo makala MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA DROO YA PILI YA “WEKA AKIBA NA USHINDE”
yaani makala yote MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA DROO YA PILI YA “WEKA AKIBA NA USHINDE” Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA DROO YA PILI YA “WEKA AKIBA NA USHINDE” mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/mwalimu-commercial-bank-mcb-yatoa.html
0 Response to "MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA DROO YA PILI YA “WEKA AKIBA NA USHINDE”"
Post a Comment