Loading...
title : NISHATI NA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UKUSANYAJI MADUHULI YA SERIKALI – GePG
link : NISHATI NA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UKUSANYAJI MADUHULI YA SERIKALI – GePG
NISHATI NA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UKUSANYAJI MADUHULI YA SERIKALI – GePG
Wizara ya Nishati na Madini imetoa mafunzo ya Mfumo wa pamoja wa Kukusanya Maduhuli ya Serikali (GePG) kwa Maafisa Madini na Wahasibu wa Wizara hiyo ili kuboresha shughuli za ukusanyaji maduhuli.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Anthony Tarimo alisema kuwa mafunzo yamelenga kuwawezesha washiriki kuuelewa vyema mfumo huo ili kuwa na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali wenye tija.
Alisema Serikali imeamua kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa maduhuli kuwa wa kielektroniki ili kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli na vilevile kuongeza uwazi miongoni mwa Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.
“Kupitia mfumo huu, Serikali inao uwezo wa kujua maduhuli yote yanayoingia kwa wakati mmoja kwa sababu umeunganishwa na Wizara na Taasisi mbalimbali,” alisema Tarimo.
Alibainisha kuwa Mfumo huo wa GePG ulianza kutumika rasmi Julai, 2017 na kwamba kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini mafunzo ya awali yalitolewa kwa watumishi wa Ofisi ya Madini- Kanda ya Mashariki ambayo inahusisha ofisi za madini za Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Handeni na Morogoro.
Alisema Mfumo huo ni rafiki na kwamba utaboresha na kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli na kwamba mara baada ya mafunzo, washiriki watakuwa na uwezo wa kuutumia ipasavyo. Tarimo alisema mafunzo hayo yanawahusu Wahasibu, Maafisa Leseni pamoja na watumishi wengine ambao kwa njia moja ama nyingine wanahusika na utoaji wa hati za madai za malipo mbalimbali.
Aliongeza kuwa, mafunzo hayo yanahusisha uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa TEHAMA wa Wizara ya Fedha na Mipango na wa Wizara ya Nishati na Madini na pia yatahusisha majadiliano ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi wanaohusika na ukusanyaji wa maduhuli.
“Wanasheria pia watawasilisha mada ili kuelewa vyema mabadiliko katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanyika hivi karibuni,” alisema Tarimo. Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyikia katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (SUA) na yameanza Agosti 28, 2017 kwa kushirikisha zaidi ya washiriki 100.
Hivyo makala NISHATI NA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UKUSANYAJI MADUHULI YA SERIKALI – GePG
yaani makala yote NISHATI NA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UKUSANYAJI MADUHULI YA SERIKALI – GePG Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NISHATI NA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UKUSANYAJI MADUHULI YA SERIKALI – GePG mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/nishati-na-madini-yaendesha-mafunzo-ya.html
0 Response to "NISHATI NA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UKUSANYAJI MADUHULI YA SERIKALI – GePG"
Post a Comment