Loading...

TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa

Loading...
TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa
link : TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa

soma pia


TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Matumizi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang'a , Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri, Samwel Mbuya, pamoja na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini Tanzania leo imewapa semina baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alisema semina hiyo ni utaratibu wa TMA kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuwa mabalozi wa zuri wa kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi mazuri ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa wananchi. 

Alisema wanahabari inabidi wazielewe vizuri, kuzichambua na kuwafikishia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kiusahihi wananchi jambo ambalo litasaidia wananchi na sekta mbalimbali kujipanga kukabiliana na ama athari zitokanazo na utabiri wa hali ya hewa. 

"...Semina kama hizi kwanza zinasaidia wanahabari kuelewa masuala mbalimbali yatokanayo na taarifa zetu za utabiri, kisha wao kuelimisha jamii zaidi kuhusiana na taarifa zetu kupitia vyombo vyao mbalimbali vya habari. Kundi hili likielewa vizuri nao watakuwa mabalozi wazuri kufikisha ujumbe kupitia kalamu zao," alisema Dk Agnes Kijazi. 

Aidha pamoja na mafunzo hayo, TMA pia ilipokea mrejesho na ushauri kutoka kwa wanahabari ili kuboresha zaidi namna ya utoaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa umma. Picha ya pamoja ya washiriki wa semina kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa.


Hivyo makala TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa

yaani makala yote TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/tma-yawajengea-uwezo-wanahabari.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TMA yawajengea uwezo wanahabari uandishi wa habari za hali ya hewa"

Post a Comment

Loading...