Loading...
title : WAZIRI LUKUVI APOKEA RASIMU YA MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI, MJINI MOROGORO
link : WAZIRI LUKUVI APOKEA RASIMU YA MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI, MJINI MOROGORO
WAZIRI LUKUVI APOKEA RASIMU YA MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI, MJINI MOROGORO
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amepokea rarmi Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na Changamoto za Matumizi bora ya Ardhi Nchini na kutaja Teknolojia kuwa ni changamoto inayokabili mpango wa matumizi bora ya ardhi inayopelekea kulegalega kwa upangaji, upimaji na umikilishaji wa Ardhi.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo mjini Morogoro wakati alipokuwa akipokea rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi nchini, iliyoonesha na kuainisha mapendekezo katika uandaaji,usimamizi na utekelezaji.
“Tunahitaji teknolojia rahisi ambayo hata ninyi mkondoka serikali inaweza kuhimili, hatupendi mtuambukize teknolojia ambayo itakuwa ni ngumu kwetu, kwakuwa serikali inapopanga gharama kubwa zinajitokeza kwenye picha za anga na zile za chini,” alisema Lukuvi.
Lukuvi alisema kuwa kuhusu fedha si tatizo lakini ukosefu wa teknolojia ndio tatizo kubwa zaidi,hivyo ni vizuri kuyatazama haya mashirika yasiyo ya kiserikali tushirikiane nayo ili yaweze kuangalia ni teknolojia gani rahisi itakayoweza kupunguza gharama za upimaji na upangaji wa ardhi vijijini baada ya kusubiri ndege za anga ambazo ni gharama kubwa.
Aliongeza kuwa Serikali inapenda kuwa na uratibu wa haraka, ulio rahisi ambao wananchi wanaweza kupanga maeneo yao na kuongeza, lakini pia kuondokana na migogoro ya Ardhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akifungua rasmi mkutano kwa ajili ya kusikiliza na kupokea Rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Changamoto za Matumizi Bora ya Ardhi Nchini, mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe akitoa maelezo juu ya mkutano huo na kuonesha namna gani itakavyoweza kumaliza migogoro ya Ardhi Nchini.
Hivyo makala WAZIRI LUKUVI APOKEA RASIMU YA MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI, MJINI MOROGORO
yaani makala yote WAZIRI LUKUVI APOKEA RASIMU YA MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI, MJINI MOROGORO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUKUVI APOKEA RASIMU YA MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI, MJINI MOROGORO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/waziri-lukuvi-apokea-rasimu-ya-mkakati.html
0 Response to "WAZIRI LUKUVI APOKEA RASIMU YA MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI, MJINI MOROGORO"
Post a Comment