Loading...
title : Azam kuna upinzani mkubwa wa makipa- Kocha Makipa Azam
link : Azam kuna upinzani mkubwa wa makipa- Kocha Makipa Azam
Azam kuna upinzani mkubwa wa makipa- Kocha Makipa Azam
KOCHA wa makipa wa timu ya Azam Fc, Idd Abubakar, amekiri upinzani mkali kwa makipa wake kikosini kwani wana jumla ya makipa wanne kikosini, Mghana Razak Abalora, Mwadini Ally, Benedict Haule na Metacha Mnata aliyepandishwa, wote wakiwa wanaunda kikosi cha timu kubwa kwenye eneo hilo.
Kwa sasa tokea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ianze Agosti 26 mwaka huu, Abalora ameonekana kuwa chaguo la kwanza, akiwa mpaka sasa hajaruhusu wavu wake kuguswa kwenye mechi zote mbili za mwanzo, Azam FC ikiifunga Ndanda bao 1-0 kabla ya juzi kutoka suluhu na Simba.
Abubakar alisema kuwa upinzani huo ulidhihirika wakati wakiwa kwenye kipindi cha maandalizi ya msimu mpya nchini Uganda, ambapo kila kipa aliyepewa nafasi aliweza kukaa imara langoni.
“Upinzani upo mkubwa sana na isitoshe vilevile baada ya kuziangalia mechi za pre season tulizocheza kila mmoja anataka nafasi, hawa makipa wote wanne wanahitaji kucheza na viwango vya vyote mazoezini na mechi wanazopewa kila mmoja mechi yake ameitendea haki.
“Tulianza mechi ya kwanza na Mwadini (Ally) amecheza vizuri tu tumekuja tumecheza na Razak (Abalora) mechi mbili amecheza vizuri kwa hiyo kiwastani kiujumla kabisa upinzani upo mkubwa sana kwamba hakuna golikipa ambaye amebweteka kwamba hapa amefika katika hii nafasi,” alisema.
Kocha wa makipa wa timu ya Azam Fc, Idd Abubakar (pili kulia) akiwa pamoja makipa wanaounda kikosi cha timu hiyo.
Hivyo makala Azam kuna upinzani mkubwa wa makipa- Kocha Makipa Azam
yaani makala yote Azam kuna upinzani mkubwa wa makipa- Kocha Makipa Azam Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Azam kuna upinzani mkubwa wa makipa- Kocha Makipa Azam mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/azam-kuna-upinzani-mkubwa-wa-makipa.html
0 Response to "Azam kuna upinzani mkubwa wa makipa- Kocha Makipa Azam"
Post a Comment