Loading...

Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari

Loading...
Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari
link : Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari

soma pia


Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari


HA
Na Masanja Mabula –Pemba
BARAZA la Mji Chake Chake Pemba limesema mabadiliko ya  kanuni katika sheria namba 7 ya mwaka  2014 sheria ya mamlaka ya serikali za mitaa yamelenga katika kuleta ufanisi wa uwajibikaji kwa wafanyabiashara na wananchi wote
Akizungumza na wafanyabiashara hao afisa  afya kutoka baraza la mji khamis Abas Machano kwa niaba ya mkurugenzi wa baraza hilo   amewataka wafanyabiashara hao  kutambua kuwa baadhi ya kanuni za kisheria zimebadilika.
Amesema baadhi ya kaununi hizo zimo zinzowagusa moja kwa moja wafanyabiashara hao, hivyo ndio  wakaona kuna umuhimu wa kuwaita na kuwaeleza kwakuwa wafanyabiashara hao ni miongoni mwa wadau wakuu wa baraza hilo
Akitaja kanuni iliyobadilika na inayowahusu wafanyabiashara hao amesema kuwa, kuanzia sasa ada ya usafi imebadilika na kuwa shilingi 1000 badala ya ile ya mwanzo waliyokuwa wakichangia shilingi 600 kwa siku.
Machano amewataka wafanyabiashara kuyapokea mabadiliko hayo kwa mikono miwili kwani hayana lengo baya bali ni kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla huku akisisitiza suala la usafi katika maeneo yao ya kazi .
Aidha amesisitiza kuwa suala la  upimwaji wa afya litafanyika kila baada ya miezi sita (6) ambapo kila  mfanyabiashara anaeuza chakula anatakiwa kupima afya yake.
“Kila mfanyabiashara anatakiwa ahakikishe anaimarisha  usafi katika sehemu yake ya biashara pamoja na kuwa na chombo maalum chenye ufuniko cha kuwekea taka, baraza halitosita kumchukulia hatua mfanyabiashara ambae hatokubaliana na masharti hayo, baraza limejipanga” alisema Machano.
Kwa Upande wake mhasibu wa Baraza la hilo ,  Khamis Ali amewasisitiza wafanyabiashara hao kutokwenda kinyume na sheria zilizowekwa kwani lengo ni maendeleo kwa wote .
Amefahamisha kuwa  kile kinachokusanywa na Baraza hutumika kwa kukirudisha kwa wanajamii wenyewe katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotekelezwa na baraza hilo kama vile ujenzi wa vyoo katika maeneo yenyeshida hiyo, ujengaji wa madarasa ya wanafunzi katika skuli na mengineyo.
Mpaka kikao hicho kinamalizika , wafanyabiashara hao walionekana kuyapokea mabadiliko hayo kwa lengo la kwenda kuyatekeleza kama sheria zinavyowataka.


Hivyo makala Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari

yaani makala yote Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/baraza-la-mji-chake-chake-pemba.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Baraza la Mji Chake Chake Pemba lazungumza na wafanyabiashara Mwambawahabari"

Post a Comment

Loading...