Loading...

CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

Loading...
CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO
link : CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

soma pia


CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam 
SERIKALI ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 29.4 kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu ya ufundi stadi, utalii wa kijiolojia na kukarabati wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Gou Haodong. 
Bw. Doto James alisema kuwa kiasi cha Shilingi bilioni 22.4 cha msaada huo kitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera, ambacho kitakapo kamilika kitadahili zaidi ya wanafunzi 400. 
“Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” alisema Bw. James. 
Alieleza kuwa kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho. 
“Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu wake watakaochangia kukuza sekta ya uzalishaji na hatimaye kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini” alisema Bw. James
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong (wa tatu kushoto) wakisaini makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 kwa ajili ya miradi ya Ujenzi wa Chuo cha VETA Mkoani Kagera, Utalii wa Kijilojia na Ukarabati wa Uwanja wa Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 kwa ajili ya miradi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA), Mkoani Kagera, Utalii wa Kijiolojia na Ukarabati wa Uwanja wa Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) hati ya makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 uliotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya miradi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) Mkoani Kagera, Utalii wa Kijiolojia na Ukarabati wa Uwanja wa Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Khamis Shaaban (kushoto) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga (kulia) wakishuhudia utiliwaji saini makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 uliotolewa na China kwa ajili ya miradi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) Mkoani Kagera, Utalii wa Miamba na Ukarabati wa Uwanja wa Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong (wa pili kulia) na Maafisa waandamizi kutoka Tanzania na China wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusainiwa makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 uliotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya miradi mbalimbali katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.  
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano 
Serikali Wizara ya Fedha na Mipango)


Hivyo makala CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

yaani makala yote CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/china-yaipatia-tanzania-msaada-wa-sh_29.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO"

Post a Comment

Loading...