Loading...
title : DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI
link : DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI
DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu leo Septemba 10, 2017 amefanya kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani ili kuwaeleza dhamira ya kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kukuza ufanisi na kiwango cha ufaulu katika Wilaya hiyo.
Katika kikao hicho wadau wamechangia jumla ya shilingi milioni 3,900,000 ikiwa ni ahadi, Mifuko 100 ya saruji na rasilimali hamasa kwa vijana wa waliohitimu masomo ya sayansi katika vyuo mbalimbali nchini watakaojitolea kufundisha katika shule zenye upungufu wa walimu sayansi katika Wilaya ya Ikungi.
Mhe Mtaturu amewaeleza washiriki wa kikao hicho namna ambavyo Uongozi wa Wilaya umejipanga kwa kuhusisha michango ya wadau na nguvu za wananchi kwa ujumla kwa kuchangia rasilimali fedha ama viwezeshi kama vile saruji, mchanga, kokoto na vitu vifaa vingine vya ujenzi.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Lamada Hotel Jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Mwalimu Athumani Salum ambaye ni Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi, Mhe Mtaturu alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu Wilayani Ikungi ikiwa ni pamoja na Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Afisa elimu Mkoa wa Dar es salam Mwalimu Khamis Lissu akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Hivyo makala DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI
yaani makala yote DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/dc-mtaturu-afanya-kikao-na-wadau-wa.html
0 Response to "DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI"
Post a Comment