Loading...
title :
link :
Jovina Bujulu-MAELEZO
Hivi karibuni, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea (TFRA) imeingiza nchini mbolea yenye uzito wa tani 55,000 kwa mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja bila kuwepo malipo ya ziada bandarini.
Mfumo huo utasaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima wengi nchini.
Uingizwaji wa mbolea hiyo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2017/18, mjini Dodoma.
DKt. Tizeba alisema kuwa kuanzia msimu wa 2017/18 Serikali itaanza kuagiza mbolea kwa mfumo wa pamoja kwa kuanza kuagiza aina mbili za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA), kwa kuwa ndizo zinatumika sana nchini.
Alitaja sababu za kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya mbolea nchini kwa kuhakikisha kuwa wadau wote wanapata uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani.
Aidha, mfumo huo unawawezesha wafanyabiashara wadogo wanapata nafasi ya kuagiza mbolea na kuimarisha mtandao wa usambazaji hadi ngazi ya mkulima.
Vilevile utaratibu huo unawawezesha waagizaji kununua mbolea wakati bei ikiwa ndogo na TFRA kufuatilia bei hiyo ili kuepuka mwanya wa waagizaji kuongeza bei zaidi ya ile iliyonunuliwa kwa bei ndogo
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/jovina-bujulu-maelezo-hivi-karibuni.html
0 Response to " "
Post a Comment