Loading...
title : KIKUNDI cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) chaomba kupigwa jeki na serikali ili kupambana na umaskini kwa vitendo
link : KIKUNDI cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) chaomba kupigwa jeki na serikali ili kupambana na umaskini kwa vitendo
KIKUNDI cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) chaomba kupigwa jeki na serikali ili kupambana na umaskini kwa vitendo
Na David John Mwanza
KIKUNDI cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) wameiomba Serikali kuunga mkono jitihada zinazofanywa na umoja huo ambapo wameamua kwa dhati kupambana na umasikini kwa vitendo.
Wamesema wao kama kikundi cha ujasiliamali wilaya ya ilemela kimebeba vikundi zaidi ya 16 ambapo wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasilimali ikiwamo ufundi nguo,Mapambo nakadhalika.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Katka ofisi za kikundi hicho Mwenyekiti wake Asile Amour.Amesema kikundi hicho kimeazishwa Mapema mapema mwaka huu na kimekusanya zaidi ya vikundi 16kutoka katika Kata ya Nyasaka wilayani Ilemela.
"Tunaiomba Serikali kutuunga mkono kwani tumeamua kwa dhati kuunga mkono serikali hususani katika sera yake ya viwanda kuona na sisi kama wanawake tunajikomboa. "amesema Mwenyekiti Asile
Amesema wamejipanga kufanya harambee kwa lengo la kutunisha mfuko wao huku akitoa rai kwa viongo wa vyama na Serikali kushiriki kuwaunga mkono kama wanavyofanya kwenye maeneo mengine.
Naye Mhazini wa kundi hilo Esther Kakwene amesema kundi lao lina wanachama zaidi ya 100 nikundi kubwa ambalo limekusanya watu kutoka kila mtaa ndani ya kata ya Nyasaka.
"Hapa tulipo tumepewa sehemu ya kujenga Ofisi kwa ajili ya kikundi chetu hivyo tunaomba viongozi wetu watusaidie ili tufanikishe malengo yetu. Kundi hili tumesajiliwa na tumepewa cheti cha utambulisho hivyo tupo kikazi zaidi. Amesema Esther.
Hivyo makala KIKUNDI cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) chaomba kupigwa jeki na serikali ili kupambana na umaskini kwa vitendo
yaani makala yote KIKUNDI cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) chaomba kupigwa jeki na serikali ili kupambana na umaskini kwa vitendo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIKUNDI cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) chaomba kupigwa jeki na serikali ili kupambana na umaskini kwa vitendo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/kikundi-cha-umoja-wa-wanawake-wilaya-ya.html
0 Response to "KIKUNDI cha umoja wa wanawake Wilaya ya Ilemela (UWN) chaomba kupigwa jeki na serikali ili kupambana na umaskini kwa vitendo"
Post a Comment