Loading...
title : MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MIRADI YA KUIMARISHA ELIMU MKOA WA KUSINI
link : MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MIRADI YA KUIMARISHA ELIMU MKOA WA KUSINI
MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MIRADI YA KUIMARISHA ELIMU MKOA WA KUSINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja kutunza miradi na kuitumia kwa manufaa ya wote.
Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa Ufunguzi wa Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi ambao umefadhiliwa na Ubalozi wa Japan.
Mhe. Samia aliwashukuru Ubalozi wa Japan kwa kufadhili ujenzi wa Uboreshaji wa Mazingira ya Elimu katika Wilaya ya Kusini ambao umegharimu dola za kimarekani laki moja na elfu kumi na mbili na mia nane na arobaini na tano (112,845) ambazo ni sawa na takribani ya shilingi milioni mia mbili arobaini na saba (247) .Awali Ubalozi wa Japan ulitoa dola za Kimarekani elfu ishirini na nane mia nane na sitini (28,860) takribani shilingi milioni sitini na moja za kitanzania kujenga uzio wa shule ya Msingi Muyuni .
Makamu wa Rais alimshukuru sana Balozi wa Japan kwa ufadhili huo ambao umeendelea kuimarisha urafiki na mahusiano kati ya nchi mbili hizi, aliwataka wananchi wa Wilaya ya Kusini kutilia mkazo masuala ya elimu na kutunza miradi yote ili inufaishe na vizazi vijavyo.
Makamu wa Rais pia aliwapongeza viongozi wa halmashauri ya wilaya ya kusini kwa kusimamia vizuri fedha za ufadhili na kufanikisha kukamika kwa ujenzi wa miradi kama ilivyopangwa na kukamilika mapema zaidi .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki lililobeba mada isemayo Kuleta Mabadiliko katika jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutumia Kiswahili lilianza leo mjini Unguja, Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ofisi ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mjini Zanzibar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakipeana ishara ya kushukuru mara baada ya Balozi wa Japan kukabidhi miradi miwili mikubwa,mmoja ukiwa ni ujenzi wa uzio wa shule ya Msingi ya Muyuni na wa pili ni mradi wa uboreshaji wa mazingira ya elimu katika wilaya ya ya kusini uliojumuisha ujenzi wa shule ya awali katika kijiji cha Kajengwa na Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakikata utepe kama ishara ya kufungua Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuelezea Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida namna Pomboo wanavyovutia utalii katika mkoa wa kusini wakati akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Pomboo mara baada ya ufunguzi wa Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MIRADI YA KUIMARISHA ELIMU MKOA WA KUSINI
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MIRADI YA KUIMARISHA ELIMU MKOA WA KUSINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MIRADI YA KUIMARISHA ELIMU MKOA WA KUSINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/makamu-wa-rais-azindua-kongamano-la.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MIRADI YA KUIMARISHA ELIMU MKOA WA KUSINI"
Post a Comment