Loading...

MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA

Loading...
MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA
link : MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA

soma pia


MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA



Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd imezindua Mradi mkubwa wa ufugaji kuku unaosimamiwa na Kikundi cha Ujasiriamali cha Shinyanga,Kishapu na Kahama (SHIKIKA) uliopo katika mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga.

Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo Jumatatu Septemba 18,2017 katika mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga.Kikundi cha SHIKIKA kinachotekeleza mradi huo,kilianzishwa Machi 16,2017 baada ya kampuni ya Namaingo Business Agency Co.Ltd kuwaelekeza wanachama wake kuunda vikundi vya wanachama hamsini hamsini ili wakubaliane kuendesha mradi wanaoupenda.

Wanakikundi hao waliamua kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji ndipo kampuni hiyo ikawachangia vifaranga 200,wakaanza ufugaji tarehe 9.6.2017 na mpaka sasa kikundi kina kuku zaidi ya 1300.Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim aliwapongeza wanakikundi hao kwa kuchangishana fedha shilingi milioni 8 na kuamua kuanzisha mradi huo.

“Ndugu zangu jambo hili mlilofanya na mlilolitekeleza kwanza ni jambo la kitaifa kwa sababu wananchi wakiwa na uchumi mzuri serikali nayo inapata kodi lakini pia tunakuwa tumetengeneza ajira”,alisema Ibrahim.

“Pamoja na jitihada hizi mlizochukua kwa muda mfupi,Tunatamani kuona kila mtu anakuwa na kuku walau 1000 kwenye banda lake,najua changamoto kubwa iliyopo ni mitaji na riba kubwa kwenye mikopo lakini kuna fedha kwa ajili ya maendeleo ya akina mama na vijana zenye riba ndogo sana zipo kwenye benki mbalimbali,serikali inafanyia kazi suala la mikopo hiyo”,aliongeza.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akishikana mkono na Katibu wa SHIKIKA,Gelard Egwaga baada ya kukata utepe.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akiangalia kuku wenye umri wa miezi miwili katika moja ya mabanda ya kundi la SHIKIKA.

Viongozi wa kundi la SHIKIKA wakimwongoza Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim kuangalia kuku hao.

Ndani ya banda la kuku,mgeni rasmi Biubwa Ibrahi na waangalizi wa kuku (vijana watatu kulia).



Hivyo makala MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA

yaani makala yote MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/mradi-mkubwa-ufugaji-kuku-wajasiriamali.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MRADI MKUBWA UFUGAJI KUKU WAJASIRIAMALI KUTOKA SHINYANGA,KISHAPU NA KAHAMA WAZINDULIWA"

Post a Comment

Loading...