Loading...

NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita.

Loading...
NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita.
link : NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita.

soma pia


NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos Makalla akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Uyole uliofanyika jijini Mbeya. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
 Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani – Augustino Mbogella akizungumza na wateja wa NMB waliokusanyika kushuhudia uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni wilayani Songwe katika mkoa wa Songwe. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.

BENKI ya NMB Imefungua matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita ikiwa ni juhudi za kujiimarisha zaidi na kuwa karibu na Wateja wake wa kanda ya nyanda za juu.

Matawi hayo yamefunguliwa katika mikoa ya Njombe, Mbeya,Songwe, Rukwa na Katavi. Matawi ambayo yamefunguliwa na yanatoa huduma kwa jamii ni pamoja na NMB  Kasumulu, NMB Uyole, NMB Mkwajuni, NMB Wanging’ombe, NMB Laela na NMB Kalambo lililopo Mlele.

Idadi hii ya matawi mapya inafanya jumla ya matawi ya NMB 31 katika kanda ya Nyanda za Juu huku yakifikia matawi ya NMB 207 nchi nzima.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la NMB Uyole lililopo mkoani Mbeya, Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu - Badru Iddy amesema kuwa lengo la Benki hiyo ni kusogeza huduma zaidi kwa wananchi ili kuwa karibu na wateja wake.

“Kuzinduliwa  kwa tawi hili la NMB Uyole mahali hapa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wetu wa Uyole kupata tawi la NMB lenye nafasi ya kutosha .Aidha  eneo hili ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wetu wakubwa na wananchi kwa ujumla. Tawi hili  kama yalivyo matawi yetu mengine nchini linatoa huduma zote za kibenki zitolewazo na benki yetu," alisema Badru.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Uyole, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya - Amos Makalla alisema kuwa Wananchi wanapaswa kufungua akaunti katika Benki hiyo na kuitumia kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 32 katika Benki hiyo.

“Hapa tuelewane, Serikali na Benki ya NMB ni sawa na mapacha kwa kuwa kila mahala ambapo serikali imepeleka huduma zake za kijamii Benki hiyo hufuatia kwa kuweka huduma za kifedha ili kuwahudumia wananchi wa eneo husika,” alisema Mheshiwa Makalla.

Huko Mkoani Songwe Mkuu wa Wilaya ya Songwe  - Samwel Jeremiah ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa huo  - Chiku Galawa kwenye uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni, aliwataka wananchi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na hivyo kutumia fursa zinazotokana na benki ya NMB kukuza uchumi wao na mwisho kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa ujumla. Alisema desturi ya kuhifadhi fedha  Benki kunajenga nidhamu ya matumizi ya fedha kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea.


Hivyo makala NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita.

yaani makala yote NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/nmb-yazinduwa-matawi-saba-kwa-mpigo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita."

Post a Comment

Loading...