Loading...
title : PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO.
link : PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO.
PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wametiliana saini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano.
Mkataba huo uliosainiwa leo Dar es Salaam, utawezesha PPRA na NEEC kushirikiana kiutendaji ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kushiriki kwenye fursa mbalimbali zinazopatikana katika manunuzi ya umma.
Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini mkataba huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima, lengo linguine ni mamlaka kuhakikisha kigezo mojawapo wakati wa hatua ya tathimini kwenye zabuni za umma cha upendeleo kwa ajasiriamali wadogo na kati kinazigatiwa.
“Pia kila mwaka PPRA na NEEC kufanya tathimini ya pamoja ili kujua namna taasisi nunuzi zinavyotekeleza au kuzingatia ushiriki wa wajasiriamali wadogo na wakati,”alisema Dk. Shirima.
Malengo mengine ni PPRA na NEEC kufanya tafiti za pamoja zitakazo jikita zaidi katika uwezeshaji na ushiriki wa wajasiriamali wadogo na kati kwenye michakato ya manunuzi ya umma.
“Suala la kuwajengea wananchi uwezo wa kupambana na umasikini kwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi limekuwa kipaumbele kikubwa cha serikali na hasa ya awamu ya tano.
Ili kufanikisha azma hiyo , serikali imekuwa ikiandaa sera na sheria mbalimbali zinazoweka mazingira mazuri ya wananchi kushiriki na kuitumia fursa za kibiashara,”lifafanua Dk. Shirima.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima,akizugumza wakati wa hafla ya utilianaji saini wa mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) leo jijini Dar es Salaam.(kushoto)ni Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’I Issa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima(kulia)pamoja na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa wakisaini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano wanaoshuhudia (kulia) ni Mwanasheria Mwandamizi wa PPRA, Agnes Sayi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Esther Mmbaga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima, pamoja na wakibadilisha hati za mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Hivyo makala PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO.
yaani makala yote PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/ppra-na-neec-zaingiia-makubaliano-ya.html
0 Response to "PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO."
Post a Comment