Loading...
title : PROF. KABUDI ATEMBELA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI
link : PROF. KABUDI ATEMBELA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI
PROF. KABUDI ATEMBELA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Prof. Palamagamba John Kabudi, ametembelea ubalozi wa Tanzania Brusels, Ubeligiji tarehe 29 Septemba, 2017. Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji Mheshimiwa Joseph Edward Sokoine.
Prof. Kabudi yuko Mjini Brussels, Ubeligiji akiambatana na Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi.
Wakati akiwa Brussels, Prof. Kabudi ameshiriki mazungumzo baina ya Rais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais wa Kamisheni ya Jumuiya ya Ulaya kuhusu Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi baina ya Jumuiya ya Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe Prof. Palamagamba Kabudi,Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya pamoja Bw. Geoffrey Kabakaki, Mwambata Maalum (Minister Plenipotentiary) wakati alipotembea makazi ya Balozi.
Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akisalimiana na Mhe. Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi za Ubalozi zilizoko Mjini Brussels, Ubeligiji
Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mhe. Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi za Ubalozi zilizoko Mjini Brussels, Ubeligiji
Picha ya pamoja
Hivyo makala PROF. KABUDI ATEMBELA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI
yaani makala yote PROF. KABUDI ATEMBELA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROF. KABUDI ATEMBELA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/prof-kabudi-atembela-ubalozi-wa.html
0 Response to "PROF. KABUDI ATEMBELA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI"
Post a Comment