Loading...

SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW)

Loading...
SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW) - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW), tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW)
link : SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW)

soma pia


SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW)

Kiwavijeshi aina ya Fall Armyworm (FAW).

Na Mathias Canal, Dar es salaam 

Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imeanza jitihada za kuwakabili Viwavijeshi wapya aina ya Fall Armyworm (FAW) wanaojulikana kitaalamu kama Spodoptera Frugiperda ambao wametajwa kuwa na uwezo mkubwa kuharibu mazao mbalimbali hususan mahindi ambayo ndio zao kuu la chakula nchini.

Imeelezwa kuwa Viwavijeshi hao wanapofika kwenye mazao hutoa kemikali ambayo huweza kudanganya mmea kuwa unashambuliwa na magonjwa kama ukungu au fangasi hivyo mmea unapohisi unashambuliwa na hayo magonjwa, hupunguza kinga dhidi ya wadudu hao hatari na kuwa rahisi kushambuliwa. 

Hayo yamebainishwa leo Septemba 14, 2017 na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Beatus Malema wakati akifungua warsha ya siku moja mbele ya Wadau wa Kilimo ambao ni Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani USAD, ONE HACKER FUND, Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), na Mradi wa WEMA .
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Beatus Malema akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja kujadili namna ya kukabiliana na mdudu aina ya Kiwavijeshi.

Mkutano ulikuwa na lengo la kujenga uelewa wa pamoja kwa ajili ya kumkabili mdudu huyo aina ya Fall Armyworm (FAW) ambaye anashambulia mazao mbalimbali nchini hususani zao la mahindi.

Alisema Athari ya viwavi jeshi haishii kuharibu majani ya mimea pekee, wadudu hao wanapokula majani na kutengeneza sumu aina ya ‘firenide’ inayodhuru mifugo inapokula majani yaliyoathiriwa.

Bwana Malema amesema tayari Serikali imechukua juhudi za awali kukabiliana na mdudu huyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya utambuzi wa mdudu huyo kwa kuwataka Wananchi kung’oa mazao na kuyachoma pindi wanapobaini uwepo wa mdudu huyo.

Pia tayari dawa tatu zimepitishwa na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kupitia Taasisi ya uchunguzi wa Viatilifu (TPRI) zinazoangamiza wadudu hao ambazo ni Duduba 450, Mupacrone 500 EC na Match Save kutoka Kampuni ya Syngenta hivyo Wananchi wametakiwa kuzitumia haraka pindi wanapoona dalili za kuwepo wa wadudu hao shambani.
Wadau wa kilimo kutoka Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, USAD, ONE HACKER FUND, Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), na Mradi wa WEMA wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Beatus Malema akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja kujadili namna ya kukabiliana na mdudu aina ya Kiwavijeshi.


Bwana Malema amesema kuwa katika kipindi cha miaka mingi Tanzania imekuwa ikikumbwa na viwavijeshi aina ya African Armywarms ambapo mara zote imekuwa ikiwadhibiti wadudu hao wanapojitokeza kwa kuwapa kiuatilifu kinachosababaisha matumbo ya wadudu hao kujaa na hatimaye kuwasababishia vifo.



Hivyo makala SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW)

yaani makala yote SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW) mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/serikali-yaanza-jitihada-za-kuwakabili.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW)"

Post a Comment

Loading...