Loading...
title : SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO.
link : SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO.
SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO.
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO-DAR ES SALAAM
SERIKALI za Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja kumaliza vikwazo vya kibiashara katika usafirishaji na uingizaji wa bidhaa katika mipaka baina ya nchi hizo mbili hatua inayokusudia kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda mara baaada ya kumalizika kwa mkutano wa pamoja yao ulioshirikisha Viongozi Waandamizi wa Serikali hizo, Wafanyabiashara na Wakulima kutoka Mataifa hayo.
Anasema katika mkutano huo Serikali ya Tanzania iliwasilisha mapendekezo 15 kwa Serikali ya Kenya yanayopaswa kupatiwa ufumbuzi, ambapo kwa upande wa Kenya waliwasilisha mapendekezo 16 ambapo kwa kiasi kikubwa hoja hizo zimekubaliwa na kupatiwa majibu yake katika mkutano huo.
Prof. Mkenda alisema kupatikana kwa mwafaka wa majadiliano hayo ni maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Mataifa hayo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhurru Kenyatta wa Kenya kwa kuwa Viongozi hao wametaka suala hilo lipatiwe mwafaka wa haraka ili kuweza kuendeleza ushirikiano na uhusiano katika nyanja mbalimbali baina ya nchi hizo.
Baadhi ya Maafisa Waandimizi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za Kilimo kutoka wakulima kutoka Tanzania na Kenya wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizotolewa na Wenyeviti wa Mkutano huo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.
Hivyo makala SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO.
yaani makala yote SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/serikali-za-tanzania-na-kenya-zamaliza.html
0 Response to "SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO."
Post a Comment