Loading...
title : Vijana wa Temeke wajitokeza kutumia fursa mradi wa MYICD.
link : Vijana wa Temeke wajitokeza kutumia fursa mradi wa MYICD.
Vijana wa Temeke wajitokeza kutumia fursa mradi wa MYICD.
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wajitokeza kujiunga na mradi wa sauti ya vijana MYICD iliyo sajiriwa mwaka 2009, ikiwa kijana ni nguvu kazi ya Taifa ambapo wanalenga zaidi umri kuanzia 15-35 na kauli mbiu ni kijana paza sauti.
Katika semina hiyo ya mafunzo yaliyofanyika ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala kwenye halmashari ya Temeke Jijini Dar es Salaam ikiwa dhumuni la mafunzo hayo ni kujua namna ya kuunda majukwaa ya vijana kuhamasisha, ushirikiano, muongozo wa vijana katika kisiasa, kiuchumi, kijamii pamoja na kidini.
Pia vijana hao wametakiwa kujitambua katika kupata sauti zao pamoja juu ya haki na mahitaji yao, kwa kujikusanya na kutoa taarifa shirikishi juu ya fursa za kimaendeleo.
Afisa maendeleo kata ya Kilakala, Mwajuma Msafiri amesema kuwa vijana hao wameupokea wito huo vizuri kwa kuchangamkia fursa hiyo na wapo bege kwa bega katika kushirikiana na vijana wenzao waishio katika mitaa mitano (5) ya kata hiyo ambayo ni Barabara ya Mwinyi, Igunga, Kilakala, Kiaembe Samaki na Yombo Dovya.
Nae Mkurugenzi Taasisi ya MYIDC, Ismail Mnikite amesema kuwa katika mradi huo unaohusisha kata nne za Halmashauri ya Temeke ambazo ni Buza, Makangarawe, Tandika na Kilakala ambapo vijana wa vikundi vya mbio za pole pole ndio waliojitokeza kujiunga na mradi ili kupata mafunzo yanayowajenga katika kuleta maendeleo hapa Nchini, vile vile ametoa shukrani za dhati Kwa wiongozi wa Halmashauri hiyo Kwa kuonyesha ushirikiano juu ya Swala hilo.
Mkurugenzi Taasisi MYICD, Ismail Mnikite akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo ulisajiriwa mwaka 2009 ikiwa ni dhumuni la kuinua vijana katika kuwanchinimafunzo na fursa mbalimbali katika kuleta maendeleo katika ofisi ya mtendaji kata ya kilakala Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Afisa maendeleo kata ya Kilakala, Mwajuma Msafiri akizungumza na waandishi wa habari kuhusu muamko wa vijana kujitokeza kujiunga na kupata mafunzo yanayotolewa mradi wa MYICD Kwa lengo la kutaka kuleta mapinduzi na maendeleo hapa nchini katika ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mradi, Kassonga Mario akitoa mafunzo kwa vijana hao katika ukumbi wa ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Vijana wa kata ya kilakala waliojitokeza kwenye mafunzo katika Ukumbi wa ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam yalioandaliwa na mradi wa MYICD ikiwa lengo ni kutaka kupaza sauti za vijana. Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii
Hivyo makala Vijana wa Temeke wajitokeza kutumia fursa mradi wa MYICD.
yaani makala yote Vijana wa Temeke wajitokeza kutumia fursa mradi wa MYICD. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Vijana wa Temeke wajitokeza kutumia fursa mradi wa MYICD. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/vijana-wa-temeke-wajitokeza-kutumia.html
0 Response to "Vijana wa Temeke wajitokeza kutumia fursa mradi wa MYICD."
Post a Comment