Loading...
title : Wakuu wa Idara za Serikali watakuwa kuwa wakweli na wawazi
link : Wakuu wa Idara za Serikali watakuwa kuwa wakweli na wawazi
Wakuu wa Idara za Serikali watakuwa kuwa wakweli na wawazi
Na Masanja Mabula - Pemba
SERIKALI ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imeanza kutekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Zanzibar kwa kugawa majukumu ya utekelezaji wa maagizo hayo kwa maofisa Wadhamini wa Wizara na taasisi za Serikali Kisiwani Pemba.
Akizungumza katika kikao cha kutathmini ziara ya Rais katika Mkoa huo , Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman amewataka wakuu wa Idara za Serikali kuwa wakweli na wawazi ili kuendana na kasi ya utendaji wa Rais kwa kuhakikisha maagizo hayo wanayafanyia kazi .
Amesema kila Wizara inapaswa kushiriki katika kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo yaliyotolewa na Rais wakati wa ziara yake mwezi uliopita katika Mkoa huo.
“Ni vyema kila mmoja anatakiwa kuwajibika kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Rais Shein aliyoyatoa wakati wa ziara yake katika Mkoa wetu , hii itasaidia kwenda kasi na Rais wetu ”alieleza.
Wakichangia katika kikao baadhi ya maofisa wadhamini wamesema tayari wameanza kuyafanyia kazi maagizo ya Rais kwa kufanya ziara na mikutano ya watendaji wa taasisi zao.
Mapema Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba Ahmed Khalid Abdalla amewapongeza maofisa wadhamini kutokana na mchango wao uliofanikisha ziara ya Rais katika mkoa huo .
Naye Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid amewasisitiza wakuu hao wa taasisi kuhakikisha wanawajibika katika kutekeleza maagizo ya Rais kwa uwazi ili wananchi wazidishe imani na serikali yao.
Hivyo makala Wakuu wa Idara za Serikali watakuwa kuwa wakweli na wawazi
yaani makala yote Wakuu wa Idara za Serikali watakuwa kuwa wakweli na wawazi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wakuu wa Idara za Serikali watakuwa kuwa wakweli na wawazi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/wakuu-wa-idara-za-serikali-watakuwa.html
0 Response to "Wakuu wa Idara za Serikali watakuwa kuwa wakweli na wawazi"
Post a Comment