Loading...
title : Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii
link : Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii
Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii
MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuwasilisha hoja mbalimbali za kufanyiwa kazi na Serikali kupitia sekta ya elimu lengo likiwa ni kuhakikisha elimu bora inapatikana nchini Tanzania.
Akiwasilisha hoja hizo mahususi 14 mjini Dodoma, Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu alisema hii ni mara ya pili kuwasilisha hoja na lengo la msingi ni kuitaka serikali kuingiza katika utekelezaji.
Bi. Katundu alisema wanaikumbusha Serikali kuhakikisha inatenga hadi asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu na pia kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha toka mapato ya ndani ili iweze kutumika uboreshaji elimu ya msingi nchini.
Alisema hoja zingine walizowasilisha Serikalini ni pamoja na kutaka utoaji wa ruzuku shuleni hali halisi ya mahitaji ya sasa na kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta hiyo.
Aidha, hoja zingine walizowasilisha kwa kamati hiyo ni kutaka kuimarishwa kwa idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, uzingatiwaji wa haki za watoto na pia kuundwa kwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu.
Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu (kulia) akiwasilisha hoja mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii jana mjini Dodoma juu ya maboresho katika sekta ya elimu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto) na katibu wake kulia wakizungumza na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana mjini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii ikiwa katika kikao na Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).
Hivyo makala Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii
yaani makala yote Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/wanachama-tenmet-watoa-hoja-nzito-kwa.html
0 Response to "Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii"
Post a Comment