Loading...
title : Watumiaji wa simu waaswa kuwa waangalifu na matapeli -TCRA
link : Watumiaji wa simu waaswa kuwa waangalifu na matapeli -TCRA
Watumiaji wa simu waaswa kuwa waangalifu na matapeli -TCRA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WATUMIAJI wa Simu na mitandao wameaswa kuwa waangalifu katika kujiepusha na matepeli wanaotumia mitandao hiyo katika kujipatia kipato.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma, Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema kuwa simu na mitandao inatakiwa kutumika kwa uangalifu zaidi ili mawasiliano yawe na tija kwa mtumiaji.
Amesema wizi katika mitandao umkeuwa ukifanyika kila siku,hivyo kila mtu akiona taarifa tofauti anatakiwa kuripoti katika vyombo vya dola ili wizi huo usiweze kufanyika na mtu anayefanya hivyo kuanza kufuatiliwa.
Mwakyanjala amesema TCRA inafanya uchambuzi wa taarifa za matukio ya usalama wa mitandao kutoka katika vyanzo mbalimbali vya nchini , kimataifa na matokeo ya uchambuzi huo kuongeza usalama wa matumizi ya mawasialiano ya simu, komputa pamoja na Internet.
Aidha amesema TCRA inafanya tathimini ya udhaifu wa mifumo ya komputa ya mitandao ya wadau wake isiweze kusambaza ujumbe wa chuki maudhi au uchochezi unapotokea kwa mtu mwingine na kinachotakiwa kufanyika ni kufuta pale aunapoona taarifa haikidhi vigezo katika mawasiliano.
Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma, Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa habari juu ya mamlaka hiyo inavyofanya kazi leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa habari wa idara ya habari MAELEZO, Fatma Salum.
Hivyo makala Watumiaji wa simu waaswa kuwa waangalifu na matapeli -TCRA
yaani makala yote Watumiaji wa simu waaswa kuwa waangalifu na matapeli -TCRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watumiaji wa simu waaswa kuwa waangalifu na matapeli -TCRA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/watumiaji-wa-simu-waaswa-kuwa.html
0 Response to "Watumiaji wa simu waaswa kuwa waangalifu na matapeli -TCRA"
Post a Comment