Loading...

Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma

Loading...
Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma
link : Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma

soma pia


Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma

Benki ya NMB Tanzania imezindua wiki ya huduma kwa wateja ambapo imeahidi kuboresha zaidi huduma kwa wateja wake wa sasa na kuwafikia wananchi ambao bado hawajapata huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja na kusema kila mwaka wamekuwa wakiboresha huduma mbalimbali ambazo zinatolewa sasa na kuanzisha zingine mpya na wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kuboresha huduma hizo.

“Kila mwaka ni mzuri sababu kunakuwa na jambo tofauti pamoja na hilo pia tupo katika nafasi nzuri kama benki namba moja Tanzania, ni jambo la kujipongeza sababu tulipo sasa sio sawa na miaka 12 iliyopita,

“Tumejipanga kuhakikisha tunaboresha huduma zetu na zaidi kidigitali ili kuahisha huduma za kifedha kuwepo karibu zaidi na wateja wetu, huduma ya kidigitali inahitaji huduma ya intrnet ambayo kwa sasa nchini ipo vizuri na simu ya kisasa (smartphone) ambazo hata gharama zake kwa sasa zipo chini," amesema Ineke na kuongeza.

“Tumekuwa tukitoa huduma boa lakini pamoja na hilo hatuwezi kuwafikia wateja wote ndiyo maana tumekuwa na mawakala zaidi ya 3,500 nchi nzima ambao wamekuwa wakitoa huduma kwa wateja wetu."

Aidha Ineke amesema moja ya changamoto ambayo benki imekuwa ikikutana nayo kwasasa ni huduma za kifedha kupatikana kupitia mitandao hivyo wateja wengine kutumia mitandao yao kuhifadhi pesa lakini wamejipanga kuja na njia mbadala ikiwa na huduma bora zaidi ambazo zitawashawishi wananchi kutumia benki kutuma fedha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akizungumza katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika hafla iliyofanyika leo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker (hayupo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akizindua Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwa kuliruhusu gari la huduma kwa wateja kuzunguka kutoa huduma maeneo mbalimbali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma

yaani makala yote Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/benki-ya-nmb-yazindua-wiki-ya-huduma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma"

Post a Comment

Loading...