Loading...
title : DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA
link : DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA
DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA
Na Mathias Canal, Arusha
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 28, 2017 amekipongeza Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) kwa kuendelea kufungua matawi mengi nchini ya kuuza pembejeo bora za kilimo.
Mhe Mwanjelwa ametoa pongezi hizo wakati akihutubia kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Tanganyika Farmers’ association (TFA) uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha.
Alisema kuwa hiyo ni ishara njema ya kuunga mkono Ilani ya Chama cha Mapinduzi na juhudi za Serikali katika kuendeleza Sekta za kiuchumi ambazo ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Alisema kuwa wwa wajibu huo, Wizara ya kilimo imeona juhudi kubwa na za makusudi za Kampuni ya TFA jinsi ilivyojipanga katika kuwahudumia Wananchi na Wakulima nchini.
Kupitia Mkutano huo Aliwaomba Wananchi wote kuendelea kuiunga mkono Kampuni ya TFA ili waweze kupata maendeleo ya haraka kwa kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo ili kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia katika kilimo cha kisasa.
Mgeni Rasmi- Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.Picha zote Na Mathias Canal
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki sala ya kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Katibu wa Kampuni ya TFA na Ofisi ya kisheria Bi Pendo Jacob mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Mwingine ni Bi Cathy Elizabeth S. Long'lway. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo kuhusu Kazi za TFA banda la TFA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, na kushoto kwake ni Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Hivyo makala DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA
yaani makala yote DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/dkt-mwanjelwa-afungua-mkutano-mkuu-wa.html
0 Response to "DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA"
Post a Comment