Loading...
title : DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA
link : DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA
DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile amefanya ziara kwenye baadhi ya vituo vitoavyo huduma za afya kwa ajili ya kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa jijini Dar es salaam.
Akizungumza lengo la ziara hiyo Dkt. Ndungulile amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuungana na Mhe. Rais wa wamau ya tano Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kutatua tatizo la dawa katika vituo vinavyotoa huduma za afya mpaka kufikia 2020.
“Mpaka kufikia hivi sasa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetenga shilingi Bilioni 262 kwa ajili ya kutatua tatizo la uhaba wa dawa nchini kutoka shilingi bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/2016 “ alifafanua Dkt. Ndungulile.
Aidha Dkt. Ndungulile amesema kuwa katika ziara hiyo amegundua kwamba vituo vinavyotoa huduma ya afya vina dawa zote muhimu isipokuwa kuna upungufu wa vifaa tiba ambapo tatizo hilo litafanyiwa kazi mara moja .
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Mwananyamala Bw. Marco Sallingu kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa pili kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za wa Hospitali ya Mwananyamala wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Sinza Palestina Bi. Doris Messanga kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa katikati waliosimama akiongea na wagonjwa wakati wa ziara yake Hospitalini Sinza Palestina alipotembelea vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Hivyo makala DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA
yaani makala yote DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/dkt-ndungulile-afanya-ziara.html
0 Response to "DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA"
Post a Comment