Loading...
title : Benki ya watu wa Zanzibar yachangia Milioni 50 Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu, Makonda, ashukuru
link : Benki ya watu wa Zanzibar yachangia Milioni 50 Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu, Makonda, ashukuru
Benki ya watu wa Zanzibar yachangia Milioni 50 Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu, Makonda, ashukuru
Benki ya watu Zanzibar (PBZ) imetoa msaada wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 50 kwa Mkuu mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ikiwa ni kuunga mkono jitihada zake za Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Mkoa huo.
RC Makonda ameishukuru Benki ya watu wa Zanzibar kwa kumuunga mkono katika kampeni yake ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu.
Makonda amesema kuwa Fedha hizo zitaenda kununua Mifuko 50,000 ya Saruji itakayoweza kufyatua Tofali zaidi ya 140,000 ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kasi ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu.
RC Makonda amesema kilichomgusa kuanza kampeni hiyo ni baada ya kubaini Walimu wanafanyakazi katika mazingira magumu
Benki ya PBZ imeweka Dawati maalumu kwenye kila Tawi la Bank hiyo kwaajili ya wananchi wanaotaka kuchangia Ujenzi wa Ofisi za Walimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Juma Ameir Hafidhi amesema kuwa wameamua kutoa mchango huo kutokana na kazi anayoifanya RC Makonda kutokuwa ya ubabaishaji hivyo wanauhakika fedha walizozitoa zitafanya kazi ikiyokusudiwa.
Amemuhakikishia RC Makonda kuwa wataendelea kumuunga mkono kwenye shughuli za maendeleo kwakuwa anafanya maendeleo bila kuangalia itikadi za kisiasa.
Hivyo makala Benki ya watu wa Zanzibar yachangia Milioni 50 Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu, Makonda, ashukuru
yaani makala yote Benki ya watu wa Zanzibar yachangia Milioni 50 Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu, Makonda, ashukuru Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya watu wa Zanzibar yachangia Milioni 50 Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu, Makonda, ashukuru mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/benki-ya-watu-wa-zanzibar-yachangia.html
0 Response to "Benki ya watu wa Zanzibar yachangia Milioni 50 Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu, Makonda, ashukuru"
Post a Comment