Loading...
title : JUMIA TANZANIA WAZINDUA KAMPENI YA SIKU YA BLACK FRIDAY KWA MIKOA SITA
link : JUMIA TANZANIA WAZINDUA KAMPENI YA SIKU YA BLACK FRIDAY KWA MIKOA SITA
JUMIA TANZANIA WAZINDUA KAMPENI YA SIKU YA BLACK FRIDAY KWA MIKOA SITA
Ikiwa imebaki takribani miezi miwili mwaka 2017 kuisha, Jumia Tanzania imejizatiti kuja na kampeni iliyopewa jina la ‘BLACK FRIDAY’ ambayo itawawezesha wateja wake kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali mtandaoni kwa punguzo la mpaka alisimia 70 kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 4 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa kampeni hiyo Meneja Mauzo wa Jumia Tanzania, Bw. Idd Mkumba amebainisha kuwa kutokana na mafanikio makubwa ya kampeni hiyo iliyofanyika mwaka jana na kushuhudia watanzania wakifanya huduma za mtandaoni ambapo takribani oda 600 kwa siku wameona ni vema kuirejesha tena kwa kishindo mwaka huu.
“Mwaka 2016 ulikuwa ni wenye mafanikio kwa upande wa kampeni yetu ya BLACK FRIDAY kwani ndani ya muda wa siku tano tuliyoifanya wateja wengi waliweza kufanya manunuzi mtandaoni. Hivyo basi kwa mwaka huu tena tumeiboresha Zaidi kwa kuongeza siku kutoka tano mpaka 11 ambapo kampeni itaanza rasmi kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 4.
Na kwa kuongezea hapo ni kwamba safari hii wateja wa Dar es Salaam hawatofaidika pekee yao kwani tumejitanua Zaidi mpaka mikoa mingine kwa mara ya kwanza na kuzifikia sehemu za Visiwani Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Musoma,” alisema Bw. Mkumba.
Na kwa kuongezea hapo ni kwamba safari hii wateja wa Dar es Salaam hawatofaidika pekee yao kwani tumejitanua Zaidi mpaka mikoa mingine kwa mara ya kwanza na kuzifikia sehemu za Visiwani Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Musoma,” alisema Bw. Mkumba.
Meneja Mauzo huyo wa Jumia Tanzania aliendelea kwa kufafanua kuwa, “Lengo kubwa la kampeni hii ni kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo na kuwarahisishia watanzania kufanya huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao mahali popote walipo huku wakiendelea na shughuli zao.
Meneja Mauzo wa Jumia Tanzania, Iddy Mkumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Black Friday utakaoweza kutoa punguzo la asilimia 70 kwa bidhaa atakayoinunua mteje kupitia tovuti ya Jumia Tanzania itakayoanza mwezi wa Novemba 24 hadi Desemba 04 mwaka huu kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mwanza,Morogoro, Mara na Zanzibar.
Afisa Masoko na Mahusiano ya Jamii wa Jumia Travel, Geofrey Kijanga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Jumia Travel inavyotoa huduma za malazi na namna walivyopunguza bei kwa msimu huu wa sikukuu leo kwenye ofisi za Jumia Tanzania jijini Dar Es Salaam
Mkutano ukiendelea kwenye ukumbi wa ofisi ya Jumia Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala JUMIA TANZANIA WAZINDUA KAMPENI YA SIKU YA BLACK FRIDAY KWA MIKOA SITA
yaani makala yote JUMIA TANZANIA WAZINDUA KAMPENI YA SIKU YA BLACK FRIDAY KWA MIKOA SITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JUMIA TANZANIA WAZINDUA KAMPENI YA SIKU YA BLACK FRIDAY KWA MIKOA SITA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/jumia-tanzania-wazindua-kampeni-ya-siku.html
0 Response to "JUMIA TANZANIA WAZINDUA KAMPENI YA SIKU YA BLACK FRIDAY KWA MIKOA SITA"
Post a Comment