Loading...

Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika

Loading...
Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika
link : Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika

soma pia


Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika

Mwambawahabari 



Wakati katibu wa oganaizesheni wa CCM, Pereira Silima akikanusha kupitishwa kwa sharti la ukazi kwa wagombea udiwani na ubunge, chama hicho kimewataka watumishi wa umma walioshinda uchaguzi katika ngazi ya wilaya kuamua moja; ajira au siasa.

Juzi, katibu wa uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema katika kipindi cha redio cha Times FM kuwa wanaogombea udiwani na ubunge mwaka 2020 watatakiwa kuwa wakazi wa maeneo wanayogombea, lakini mara moja akapata maswali kutoka kwa wanachama.

Lakini jana, Silima alisema CCM haiwezi kuweka sharti hilo kwa kuwa linakiuka Ibara ya 67 (1 a-c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inaeleza sifa za mtu ambaye hatakuwa na sifa za kugombea, hali kadhalika Sheria za Uchaguzi.

“Nikiwa katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa mwenye dhamana ya uchaguzi, napenda kuwajulisha kwamba Chama cha Mapinduzi kimefanya mabadiliko katika katiba yake,” anasema Silima.

“Mabadiliko ambayo yamepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliofanyika 12/03/2017, pamoja na kanuni za uchaguzi wa chama na hakuna mahali popote palipoandikwa kuwa wagombea wa udiwani na ubunge watajadiliwa kwa sifa ya kuishi jimboni.”

Silima amewataka wanachama kuzipuuza habari hizo.

Katika hatua nyingine, makamu mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula amewataka watumishi waliogombea na kushinda nafasi za uenyekiti na ujumbe wa wilaya, kuchagua moja; ajira au uongozi.

Katika toleo la juzi la Uhuru, gazeti la chama hicho tawala, Mangula amekaririwa akisema CCM itawashughulikia watendaji wake pamoja na watu ambao walikiuka maelekezo ya waraka unaozuia watendaji wa Serikali kuwania uongozi ndani ya chama.

Mangula alisema baadhi ya wilaya na mikoa ilikiuka kwa makusudi waraka huo kwa kutoa tafsiri potofu kama vile kueleza nafasi zilizozuiwa ni za utendaji, jambo ambalo alidai si kweli.

Mangula amekaririwa akisema waraka huo umeeleza bayana kwamba watumishi wa Serikali hawaruhusiwi kuwania uongozi ndani ya chama. Alisema katika hali ya kushangaza, baadhi ya watendaji kwa kushirikiana na wajumbe wengine wa vikao vya uteuzi, wamewapitisha na wengine wameshinda nafasi mbalimbali.

Alisema CCM inaliona hilo kama tukio la uvunjaji wa kanuni za maadili ya uongozi na hivyo inawataka wahusika kuanza kuwajibika kabla ya kusubiri uamuzi wa vikao vya juu.

Mangula alisema chama kinaweza kuchukua uamuzi wa kufuta matokeo ya uchaguzi katika baadhi ya wilaya kitakapojiridhisha kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni kwa kuwa suala la rushwa ni kinyume na maadili ya viongozi wa CCM.


Hivyo makala Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika

yaani makala yote Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/katibu-ccm-apinga-sharti-la-kutaka-kila.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Katibu CCM Apinga Sharti la Kutaka Kila Mgombea wa CCM Sharti awe Mkazi wa Eneo Husika"

Post a Comment

Loading...